Tuesday 15 July 2014

MALEZI YA WATOTO

Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii adimu ya kuwaandikieni makala hii fupi. Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji  wangu wapendwa kwa kuendelea kunitia moyo kwa ushauri na maoni yenu mazuri, naomba muendelee na moyo huo na nawaombeni muwaalike na marafiki zenu kusoma makala za blogu hii.
Leo naomba niongelee jukumu la malezi ya watoto ni la nani? Je, ni la Baba, Mama, Baba na Mama, Walimu, Viongozi wa dini au ni la jamii. Watoto ni zao la ndoa yaani; ni matokeo ya msichana/mwanamke na mvulana/mwanaume walioamua kuungana kama mke na mme. Japo kutokana na kukosekana kwa maadili katika jamii kuna watoto wanapatikana nje ya ndoa.
Baba; Katika jamii za kiafrika na jamii zingine pia mwanaume ndio kichwa cha nyumba. Na mara nyingi uwajibika kwa kuhakikisha mahitaji yo yote ya nyumbani yaani; chakula, mavazi na malazi yanapatikana. Lakini inapotokea mtoto kafanya makosa kazi ya kumuadibisha mtoto linaleta ugomvi miongoni mwa wazazi hao yaani; utasikia mama akigomba kwa kusema muache mtoto wangu hujui nilivyoteseka “labor” nakadhalika. Hili si sawa hata kidogo. Kwa sababu lengo ni kumweka sawa mtoto kimaadili.
Mama; Katika jamii za ki-afrika mwanamke/mama ubeba jukumu la malezi ya watoto kuanzia mimba mpaka mtoto.Malezi ya mama hujikita kwenye masuala ya kuhakikisha wamekula, wanavaa nguo safi, wanalala mahali pazuri nakadhalika. Lakini hujiepusha sana na kuadhibu watoto wanapokosea na jukumu hilo kulipeleka kwa baba lakini kwa tahadhari kubwa. Nimetumia neno tahadhari kwa maana kwamba mtoto inapotokea kaadhibiwa huwa tena wa kwanza kuomba asiadhibiwa sana na baba na hivyo kuonekana wanamapenzi na urafiki sana ya watoto kuliko baba. Lakini tabia hii si kwa akina mama wote. Baadhi ya akina mama ni kubeba jukumu la malezi kikamilifu yaani; uchukua jukumu la kuadhibu watoto inapobidi bila kusita badala ya kumpa baba jukumu hilo.
Baba na Mama; Jukumu la baba na mama ni kuhakikisha watoto wanaandaliwa mahitaji yote muhimu ya kimaisha ya kila siku aidha na yeye mwenyewe au kwa kumtumia mfanyakazi wa nyumbani. Pia na kuhakikisha kwamba watoto wanalelewa katika maadili yanayokubalika kifamilia na kijamii. Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu bora na maadili ya kidini kwa mujibu wa imani yao au ya mmoja wao.
Walimu; Wanachukua nafasi muhimu sana katika malezi ya watoto kuanzia elimu ya chekechea hadi chuo kikuu. Hawa wana nafasi muhimu sana katika kuhakikisha kwamba wanamuandaa mtoto kwa maisha ya kujitegemea kwa kumpatie utaalamu wa kumuwezesha kuendesha maisha yake kwa manufaa yake na taifa kwa ujumla. Lakini wazazi pia wanatakiwa kuwasaidia walimu kuhakikisha kwamba yale wanayofundishwa watoto wana yazingatiwa na yanaeleweka na watoto.
Kwa bahati mbaya baadhi ya walimu siku hizi wamekengeuka na wanaonekana kuchangia katika kuharibu watoto wakiume na wakike kwa kutembea nao. Yaani; baadhi ya walimu wakike na wanatembea na wanafunzi wakiume na walimu wakiume wanatembea na wanafunzi wakike.
Viongozi wa dini; Wanachukua sehemu muhimu ya kuwajenga watoto ki-imani kutegemea na imani ya wazazi wao kwa Mungu wanaomwamini.
Lakini kwa bahati mbaya baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kinyume na haya mpaka kufikia hatua ya kutembea na watoto wa waumini wao. Hili si sawa hata kidogo linahitaji kukemewa na jamii.
Jamii; Jamii inawajibu mkubwa sana katika malezi ya watoto kwa sababu watoto ni zao la jamii. Lakini kutokana na jamii kukengeuka jambo hili aliko sawa na linavyotakiwa kuwa. Katika jamii ya leo, hakuna mzazi anayepata ujasiri wa kumuonya/kumuadhibu mtoto asiye wake kwa sababu ya kuogopa kutukanwa na mtoto au kuchukuliwa hatua na mzazi wake.
Katika jamii ya leo sio ajabu kuona mama au baba mtu mzima akitembea na mtoto wa jirani yake au wa kwake. Hili si sawa hata kidogo linahitaji kukemewa na jamii.
Mshirikisheni Mungu katika malezi ya watoto wenu kwa sababu ni tunu mliyopewa kwa kusudi maalumu. Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala zenye maarifa tele ya masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.






No comments:

Post a Comment