Monday 7 July 2014

CHANGAMOTO ZA KUPATA MCHUMBA KATIKA JAMII

Habari za leo ndugu wasomaji wa blogu hii. Nina imani nyote kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi hamjambo na ni wazima wa afya na kama kuna ambaye afya yake si njema Mwenyezi Mungu atanijalia atapona muda si mrefu.
Siku ya leo nitaongelea changamoto za kupata mchumba katika kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya Sayansi na Teknolojia. Uchumba ni mahusiano baina ya mwanaume na mwanamke kwa lengo la kufunga ndoa na kuwa mke na mme baada ya kila mmoja kuridhika na mwenzake. Katika makala ya utambulisho wa blogu hii kuna maelezo yenye kujitosheleza zaidi kuhusiana na neno hili.
Kwa siku za hivi karibuni kuna malalamiko ya kila upande yaani; wanaume na wanawake kuhusiana na suala la uchumba kwa kwamba wanaume hawataki kuoa na wanawanake hawataki kuolewa.  La kujiuliza tatizo ni nini hapo?  Kimsingi sababu zipo nyingi  sana na baadhi ni kama zifuatavyo : -
1)   Tabia.
2)   Tamaa.
3)   Kukosekana kwa sifa alizoziweka.
4)   Kukosekana kwa maadili katika jamii.
Ufafanuzi wa sababu hizo hapo juu na ni vipi zinachangia changamoto za kupata mchumba na hatimaye ndoa ni kama ufuatavyo:
Tabia; Ni kipengere muhimu sana kinachoangaliwa wakati wa utafuta wa mchumba yupi anafaa katika jamii. Msichana/mvulana mwenye tabia nzuri jamii inayomzunguka ndio inayomnadi msichana/mvulana mwenye tabia inayokubalika katika jamii. Yaani; “ule usemi wa kizuri cha jiuza na kibaya cha jitembeza” ujidhihilisha bayana katika hili. Kwa maana hiyo, suala la kupata mchumba kwa msichana/mvulana mwenye tabia inayokubalika katika jamii kunakuwa hakuna shida hata kidogo kwa maana kina mtu utamani kuwa mchumba wa msichana/mvulana husika. Kwa bahati mbaya hili uwahusu sana wasichana kwa kwa sababu wao ndio wanaoombwa uchumba na wanaume.
Tamaa; Kuna tabia inayoendelea kujengeka siku hadi siku ya mali kuwa ni kigezo cha kukubaliwa kuwa mchumba wa mtoto wa familia fulani au la.  Sasa katika familia binti anapomwambia mzazi wake kwamba nimepata mchumba swali la kwanza analoulizwa mtoto ni anafanya kazi gani, au ana mali gani badala ya kuuliza kama wanampendana au la. Na ikibainika kwamba anayetafuta uchumba kwa binti hana kitu hiyo inakuwa ni sababu ya kukataliwa kuwa mchumba wa binti yao.  Kutokana na sababu hiyo mabinti wengi sana wamezuiliwa kuwa wachumba wa wanaume waliyowapenda kwa dhati ya mioyo yao.  Kwa jamii za zamani mtoto anaposema amepata mchumba suala la kwanza lililokuwa linafanywa na wazazi ni kuanza kuchunguza ukoo husika una magonjwa gani ya kurithi, ukoo huo una taswira gani katika jamii nakadhalika.
Kukosekana kwa sifa alizoziweka; Kuna tabia iliyojengeka kwa baadhi ya wanawake na wanaume kupanga vigezo vya mme/mke anayetaka kuwa mchumba wake ambavyo mara nyingi ina kuwa ni vigumu sana kuvifikia vyote.  Vigezo/Sifa kama vile mrefu, mwembamba, maziwa makubwa/madogo, tabia nzuri, elimu ya kiwango fulani nakadhalika. Kimsingi ni kwamba huwezi kupata sifa zote hizo kwa mtu mmoja ni vigumu sana. Katika harakati ya kutafuta mchumba mwenye sifa hizo zote mara nyingi hujikuta wakikosa kupata mchumba kwa wakati muafaka na hatimaye kuamua kuolewa/kuoa mtu ambaye hawaendani na hana sifa hata moja kati ya hizo. Hivyo kujikuta wakiwa kwenye ndoa bila kuwa na furaha wala amani moyoni wao baada ya kuona wakati hauko upande wake.
Kukosekana kwa maadili katika jamii; Kutokana na kukosekana kwa maadili wanawake na wanaume wengi hufanya vitendo visivyo na maadili katika jamii kama vile ufuska, ulevi, nakadhalika na kuona suala la kuwa na mchumba si la lazima. Hii ni kwa sababu unapovunjika unaleta hasara na lawana nyingi na hata kifo/vifo kwa wahusika
Mshirikishe Mungu katika mipango ya maisha yako yote kwa maana yeye ndiye mwenye mpango mkakati wa maisha yako hapo duniani.  Na pia nakushauri kujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala zenye maarifa makini ya masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


No comments:

Post a Comment