Friday 11 September 2015

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA mwendelezo

Samahani sana sana wasomaji wangu wa blog hii kwa kutokutoa makala kila juma kama inavyopaswa. Hii inatokana na sababu mbalimbali za kimaisha za hapa na pale. Naomba mnisamehe kwa kutoonekana kwa kipindi kirefu bila kuwataarifa. Leo naendelea na mada niliyoicha huko nyuma.
3. Kumtafuta mchumba kumtarajiwa
Ili kumpata mchumba mzuri miongoni mwa marafiki zako wa kike/kiume ni vizuri kutokuonyesha mapema kwamba dhamira yako ya kumtafuta urafiki dada/kaka huyu ni kwa nia ya kumtafuta uchumba. Hili ni muhimu, ili asiweze kuficha baadhi ya tabia zake zisizofaa kuwa mchumba na hatimaye kuwa mke/mme.  Tabia hizo ni kama vile dharau/lugha chafu kwa wazazi ,kwa ndugu, marafiki, mchumba, uchafu n.k. kutokuwa mchaa Mungu wa dhati, uwongo, mchonganishaji,umbeya,  umalaya, kuthamini mali kwa kupitiza kiasi cha kukosa utu, nakadhalika.
Ukipata mchumba mwenye sifa tajwa hapo juu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu utakuwa umepata mchumba bora wa kuweza kuwa mke. Pamoja na sifa zote hizo mchumba mzuri/bora ni yule unayejisikia raha na fahari kuwa nae hata kumtambulisha kwa ndugu na marafiki.  Yaani, awe nakidhi matamanio yako ya mchumba  wa ndoto yako.
Nakaribisha maoni yenu ndugu wasomaji wa blog hii.

Wednesday 29 April 2015

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA- mwendelezo

1.       Kumuomba Mungu Akupatie Mchumba.
Ukweli usiyopingika kwamba watu wengi wanajua kuombea chakula au kuomba Mungu pale wanapoona kuna dalili ya hatari mbele. Maombi ya chakula huwa ni ya juu juu tu kwa sababu ni ya mazoea lakini maombi ya kumuomba Mungu pale unapohisi/kuona hatari huwa ni yahisia sana na yenye unyenyekevu na kujitoa ndani yake.
Katika maombi ya kumuomba Mungu kukupatia mke hayapaswi kuwa ya juu juu hata kidogo bali yanapaswa kuwa maombi ya kujitoa sana kwa sababu maisha ya binadamu yo yote yanaweza kujengwa au kuharibika kutegemea kapata mke au mme mwenye kufanana nae kinahisi na matarajio au la. Mali na vitu vingine vyote mtu hupewa na wazazi wake bali mke mwema hupewa na Mungu. Sentensi hiyo ya mwisho ni kwa mujibu wa maandiko mmojawapo wa vitabu vya Mungu.
Maombi ya kuomba mke kwa Mungu yanapaswa kuwa ya kujitoa yenye kuonyesha unyenyekevu mkubwa na kufunga na ikiwezekana kuwashirikisha na watu ambao mna Imani moja. Katika maombi unashauriwa kuainisha sifa unazotaka awe nazo mchumba wako zenye kurithisha matamainio yako.
2.       Kutafuta rafiki ambaye anaweza kuwa mchumba mtarajiwa.
Kikawaida kwa mujibu wa maandiko ya vitabu vitakatifu atafutae uona na ombae hupewa.  Ukiisha kumuomba Mungu atakupatia macho ya kuona kile ulichokiomba yaani; msichana/mwanamke au mvulana/mwanaume wakukufaa kuwa mchumba na hatimaye kuwa mke/mme. Kwa urahisi wa kufanya uchaguzi wa mchumba anayefaa au unayefanana naye ni vizuri ukawa na ukaribu/urafiki na wavulana/mwanaume au wasichana/wanawake wengi. Urafiki huu ni vizuri ukawa ni urafiki wa kaka na dada pasipo makubaliano yo yote yakutaka kuwa wachumba miongoni mwa marafiki hao bila shaka yo yote Mungu atakuonyesha ni yupi unayefanana nae na wakukufaa kuwa mchumba wako.
Ili kupata uchaguzi bora wa kitu cho chote ni lazima uwe na wigo wa kufanananisha kati ya hiki na kile kipi ni hivyo hivyo pia katika masuala ya uchumba.
Makala ijayo tutaendelea na ufafanuzi wa vipengere vingine

Friday 24 April 2015

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA

Habari za siku nyingi ndugu zangu wapenzi wa wavuti hii. Bila shaka kwa uwezo wa mwenyezi Mungu ni wazima na buheri wa afya.
 Leo napenda kuongelea mchakato wa kupata mchumba. Katika maisha ya hivi sana kuna changamoto nyingi sana kwa vijana hata watu wazima wanaohitaji kupata wenzi wao wa maisha. Changamoto hii, inakuja kutokana na kutokujua ni mchakato gani wapitie katika zoezi hili la kutafuta mchumba/mwenza wake wa maisha. Mchakato kwa tafsiri isiyo rasmi ni mtiririko wa matokeo ili kuweza kufikia hatua iliyokusudiwa. Mchakato wa kupata mchumba kwa watu makini ni kama ifuatavyo kwa mpangilio:-
1.       Kumuomba Mungu akupatie mchumba.
2.       Kutafuta rafike ambayo anaweza kuwa mchumba mtarajiwa
3.       Kumtafuta mchumba mtarajiwa
4.       Kupata mchumba mtarajiwa
5.       Kumshukuru Mungu kwa kukupatia mchumba
6.       Msichana/Mwanamke kuwajulisha wazazi wake kwamba amepata mchumba
7.       Mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi wa mwanamke kuchumbia
8.       Kuoana
Ufafanuzi wa kila hatua utafuata kwenye mwendelezo wa makala hii wiki ijayo.
Nakuomba uwaalike marafiki na nduguzo kutembelea wavuti hii, ili kupata maarifa ya masuala ya uchumba na mahusiano.