Friday 29 April 2016

MWALIKO

Tembelea mara kwa mara mara wavuti hii: http://tumaini-mahusiano.blogspot.com

MAMBO SITA (6) YANAYOWATIA HOFU WANAWAKE KATIKA NDOA


Karibu ndugu wasomaji wa wavuti hii, leo napenda kuongelea mambo sita yanayowatia hofu wanawake kwa waume zao pamoja ustawi wa ndoa zao. Kutokana na tafiti mbalimbali na uzoefu wa kimazingira kuna hofu nyingi wanazokuwa nazo wanawake dhidi ya waume zao hasa kwa ndoa changa na ambazo hazikupitia hatua ya uchumba wa muda mrefu. Kama iliyohada mke na mme hukutana wakiwa wote ni watu wazima waliyokulia katika mazingira, utamaduni na familia tofauti wakapendana na kufikia maamuzi ya hiari ya kufunga ndoa. Kutokana na mzingira, makuzi, utamaduni, mtazamo n.k. watu wanapokuwa wameamua kufunga ndoa hutokea hofu za kimahusiano za hapa na pale ambazo kila mmoja hujitahidi kuziondoa. Tafiti za kisaikolojia zinasema hujengwa katika mtazamo hasi. Baadhi ya hofu hizo ni kama zifuatazo: -

©       Hofu ya kutoridhishwa katika tendo la ndoa.

©       Hofu ya kutomridhisha mmewe katika tendo la ndoa.

©       Hofu ya mmewe kupotea hamu ya ndoa.

©       Hofu ya mmewe kumkinai na kuanza michepuko.

©       Hofu ya mmewe kutobadilika katika baadhi ya matendo yasiyompendeza.

©       Hofu ya kutokua kiroho kama wanandoa.

Naomba nifafanue kidogo juu ya hofu hizo sita hapo juu.

©       Hofu ya kutoridhishwa katika tendo la ndoa na mmewe.

Kutokana tafiti na ushahidi wa kimazingira ndoa nyingi zinazofungwa sasa zinakutanisha wanandoa wenye uzoefu wa viwango tofauti wa tendo la ndoa ambao wameupata kwa wanaume wengine tofauti na mme anayefunga nae ndoa. Hii inatokana na jamii kukosa maadili ya ki-utamaduni na kidini upande wa malezi.

Wanawake wengi wanaingia katika ndoa kwa kufuata hali ya uchumi ya muoaji au kutokana na umri kuwatupa mkono na hivyo kujiingiza katika ndoa na shinikizo hizo mbili, kwa sababu wenye kukidhi haja za tendo la ndoa hawahitaji kuwaoa au ni waume wa watu. Kutokana na uzoefu wa kukutana na wanaume mbalimbali na wengi kutokidhi haja zao za tendo la ndoa huingia katika ndoa na hofu hii. Tafiti zinaonyesha kwamba mwanamke akitembea na wanaume kumi ni mmoja au sifuri wenye uwezo wakumridhisha katika tendo la ndoa. Na hii ndio inayowafanya kuingia katika ndoa na hofu hiyo, licha ya kwamba asilimia kubwa ya ndoa za siku hizi wanandoa wengi huingia kwenye ndoa wakiwa wanajuana vizuri. Lakini huingia kwenye ndoa kwa  kutegemea kwamba wenza wao watabadilika na kuweza kuwaridhisha kadri watakavyoendelea kuishi.

©       Hofu ya kutomridhisha mmewe katika tendo la ndoa.

Kama nilivyongea kwenye kipengele cha hapo juu ya uzoefu wa kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Pamoja na uzoefu wa kuachwa na wanaume mbalimbali zikiambatana na kashfa mbalimbali kutoka kwa wanaume waliyowaacha huwajengea hofu ya kukidhi haja ya waume zao ya tendo la ndoa. Na kwa wanandoa ambao hawaongelei kabisa juu ya tendo hilo na hawana maandalizi kabla na tendo la ndoa huishi katika hofu hiyo maisha yao yote.

Hii ni changamoto kubwa sana katika ndoa nyingi dunia nzima, ndio talaka zinazidi kuongezeka.

©       Hofu ya mmewe kupoteza nidhamu ya ndoa.

Kawaida ukiwa katika ndoa kuna nidhamu ambayo lazima izikatiwe kama vile muda wa kurudi nyumbani, matumizi, ulaji nakadhalika kwa ndoa ambazo wanandoa wanaheshimiana. Katika ndoa ambayo wanandoa wanheshimiana kila mmoja ni mlinzi wa mwenzie yaani kuagana na kujulishana kila mmoja alipo inakuwa ni jambo la kawaida kabisa.

Kutokana na ndoa nyingi kupoteza nidhamu mme kulala nje, kuchelewa kurudi nyumbani n.k. wanawake wengi huwa na hofu ya ndoa zao kuingia katika misukosuko ya aina hii.

©       Hofu ya mmewe kumkinai na kuanza michepuko.

Kutokana na hofu ya kutokumridhisha mmewe hofu ya kukinaiwa na mmewe hujitokeza.

©       Hofu ya mmewe kutobadilika katika baadhi ya matendo yasiyompendeza.

Kutokana na sababu ya kuingia kwenye ndoa kutokana shinikizo nilizozitaja hapo juu, wanandoa wengi hugundua kwamba wenzio wao mara nyingine wanatabia ambazo ni kero kama vile ubishi, uchelewaji kurudi nyumbani bila taarifa, kufanya mambo ya msingi bila kumshirikisha mwenza, kutopenda kula nyumbani n.k. Mambo haya kimsingi huleta msongo wa mawazo pale ambapo mme anaambia kujirekebisha lakini anakuwa mgumu kubadilika kwa sababu ya tabia za mfumo dume.

©       Hofu ya kutokua kiroho kama wanandoa.

Katika nchi hasa za ki-afrika kuna ndoa za aina tatu(3):

 ü  Kidini

ü  Kiserikali

ü  Kimila

Tafiti zinaonyesha kwamba ndoa nyingi zinafungwa kidini, kutokana na hofu nilizozitaja hapo juu suluhisho pekee linategemea imani ya wahusika. Hili kutatua matatizo hayo hapo hali ya imani ya kidini ya wanandoa ni muhimu sana kwa maana taasisi hii mwanzilishi ni Mungu mwenyewe kwa mujibu vitabu vya kidini. Kwa hiyo, Imani inapokuwa chini ni vigumu sana kutatua hofu zinazojitokeza katika taasisi hii muhimu sana.

Nimeongea kifupi kwenye kila kipengele na ninaamini kila jambo linasuluhisho katika dunia hii. Naomba nipate maoni yenu.

 

 

 

 

 

 

 

Thursday 28 April 2016

UMUHIMU WA KUWA NA FAMILIA BORA ILI KUJENGA JAMII BORA.


Habari mpenzi msomaji wa wavuti hii? Na karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza umuhimu wa kuwa na familia bora ili kujenga jamii bora. Bila familia bora hakuna jamii bora ambayo italeta maendeleo katika dunia. Tunapenda kujifunza mambo ya familia au tunasoma mambo ya familia kwa sababu kuu mbili;
Kwanza, sisi sote tumezaliwa katika familia. Hakuna mtu hapa duniani ambaye hajazaliwa katika familia ndio maana sisi sote tumezaliwa katika familia na tunapaswa kujifunza sana mambo ya familia.
Pili, familia ni msingi wa maisha ya mtu. Kila mtu anapata msingi wa maisha kutoka katika familia yake. Baba na mama wakimpatia mtoto msingi mzuri wa maisha yake basi mtoto atakwenda kujenga jamii iliyo bora kabisa. Ndio maana watu wako tofauti sana hii ni kutokana na kila mtu amepata msingi wa maisha tofauti na kuna wengine wamepata msingi mzuri wengine wamepata msingi mbaya.


Kwa kawaida familia inajengwa na baba, mama na watoto au mtoto. Familia ni kiungo cha msingi katika jamii. Mungu amepanga kila mtu kuzaliwa katika familia. Mtoto anajenga maadili na mtazamo wake kuhusu yeye mwenyewe, ulimwengu na maisha kutoka katika familia kulingana na mazingira alipozaliwa na alipokulia.
Ili tujenge jamii bora tunatakiwa kwanza tujenge familia bora kwa sababu kila mtu ametokea katika familia. Ndani ya familia baba na mama wanapaswa kuwafundisha watoto maadili mema tokea wakiwa wadogo kuwa mafunzo ya jinsi kuishi, kuwa na maadili mazuri. Mtoto akikosa kupewa upendo katika familia na kufundishwa falsafa hii kubwa ya upendo atakwenda kutengeneza jamii mbovu kama mtoto anatoka katika familia ambayo baba na mama wanaishi maisha ya uadui, ugomvi yaani kama vile maisha ya chui na swala. Mtoto anaona baba na mama wanapigana tokea akiwa mdogo je unafikiri anajenga nini katika akili yake? Baba ni mlevi wa kupindukia, wazazi wote wawili wanakosa upendo, hawaheshimiani wanatukanana mbele ya watoto, nyumba haina amani kila mtu na mambo yake matokeo yake wazazi wanapandikiza chuki kwa watoto matokeo yake ni kujenga jamii mbovu.
Familia ikiishi katika falsafa ya upendo tutajenga jamii bora yenye upendo. Upendo wa kujipenda wewe mwenye na watu mwingine. Familia ikikosa kuishi katika msingi imara wa upendo wanakwenda kujenga jamii ambayo haina hofu na mtu ambaye hana hofu atafanya kitu chochote anachojisikia na kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kutokua na upendo hakuna huruma ya Mungu watu wanatenda mambo ya ajabu ambayo chanzo chake ni kukosa msingi bora kutoka katika familia.
Familia inayowajibika katika kufanya kazi kwa bidii, kila mmoja kutekeleza wajibu wake bila shuruti itajenga jamii bora. Familia kuwafundisha watoto kuwajibika ni mafanikio ya familia kuongeza kizazi kingine bora ambacho ndio jamii. Bila familia hakuna jamii. Jamii inapata faida kupitia familia, jamii inapata watu wanaowajibika kutoka katika familia. Familia ni mali ya jamii. Familia ikiwa nzuri na jamii itakua nzuri. Hivyo basi, familia ikiharibika na jamii inaharibika.
Watoto wanaathirika sana kisaikolojia wakiangalia matendo mabaya kutoka kwa wazazi. Mwisho wa siku watoto wanawachukia wazazi kwa matendo yao , watoto wanakata tamaa ya maisha na kuona hakuna sababu ya kuishi je kama familia imejengwa kwa msingi kama huu tutatengeneza jamii iliyo bora?

Mtu anafahamika katika jamii kama mtu wa familia fulani. Mtoto wa familia fulani na mzaliwa wa sehemu fulani. Kwa hiyo, familia inakuwa chanzo cha kujenga maisha ya mtu na familia ni muhimu sana katika malezi.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

10 Simple Steps to Change Your Eating Habits - For Dummies

10 Simple Steps to Change Your Eating Habits - For Dummies

Monday 25 April 2016

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA mwendelezo



Habari za siku nyingi ndugu zangu wasomaji wa wavuti hii. Samahani sana kwa ukimya wa muda mrefu sana, kwa sababu ni siku nyingi sana nimeanza makala hii, naomba leo niimalize kwa kuiongelea kwa kifupi ili tuendelea na makala zingine. Michakato inayofuatia ni kama ifuatavyo: -

4.      Kumshukuru Mungu

Ki-imani tunaamini kwamba mke/mme mtu hupewa na Mungu hasa kama umemshirikisha/ulimuomba kama mchakato unavyoeleza hapo juu. Na hii, ni kwamba kuoa/kuolewa ni mpango wa Mungu wa kuongeza kizazi cha wanadamu.

5.      Msichana/Mwanamke kuwajulisha wazazi wake 

Baada ya kumshukuru Mungu na kuafikiana kwenda kuwajulisha wazazi juu ya azma ya kuwa mke na mme hatua inayofuta ni msichana/mwanaume kwenda kuwajulisha wazazi juu ya suala la kumpata mwenza.

6.      Mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi wa mwanamke kuchumbia

Hatua ya mwisho ni wazazi wa mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi wa msichana/mwanaume kwenda kuchumbia ili hatimaye waweze kufunga ndoa.

Naomba nipate maoni yenu kuhusu makala husika.