Friday, 19 May 2017

MAZOEA SABA (7) MABAYA KWA WANANDOA

Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu baadhi ya mazoea mabaya ustawi ndoa ambayo hufanywa na wanandoa wengi. Pia napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu kusoma makala zangu ambazo huwa natoa kila wiki.
Leo nitaongelea makosa saba (7) ambayo mara nyinyi hufanywa na wanandoa na kusababisha kuibuka kwa migogoro katika mahusiano. Makosa hayo ni kama yafuatavyo: -
1.   Kususia tendo la ndoa bila sababu ya msingi; Tendo la ndoa ni mmojawapo wa nguzo muhimu ya ndoa zote. Kwa hiyo, inapotokea mmoja wa wanandoa kuamua kumnyima mwenzake tendo la ndoa bila sababu ya msingi ni tendo ambalo linaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa bila kujali ni ya kidini, kimila au kiserikali.
2.   Kumsema vibaya mwenzako wako kwa rafiki/ndugu; Ni makosa makubwa sana kwa mustakabali wa ndoa kwa mmoja wa wanandoa kumsema vibaya mwenzake kwa rafiki zake au ndugu zake badala ya kumuelimisha ili kuondoa  kasoro unazoziona kwake.
3.   Kutotimiza yale unayosema; Ni kosa kubwa sana kwa mwanandoa kutotimiza/kutenda yale anayoahidi kwa mkewe/mmewe bila sababu ya msingi. Katika mahusiano hutokea misukosuko ya hapa na pale na nyingi hutokea mmoja wa wanandoa kuomba msamaha na kukiri kutorudia vitendo fulani ambavyo ni kero kwa mwenzako kwa mfano; kulala nje, kuchelewa kurudi nyumbani bila taarifa yo yote, nakadhalika.
4.   Kutokukubali makosa; Ni busara kwa mstakabali mzuri wa ndoa kukubali makosa inapotokea kuwa mmoja wa wanandoa kafanya makosa. Imekuwa ni vigumu sana kwa wanandoa hasa wanaume kukubali makosa inapotokea wamefanya makosa na badala yake huonyesha kukiri kwa vitendo yaani; kufuata mapendekezo ya wake zao na siyo kukubali kwamba maamuzi yao ya awali yalikuwa na makosa. Si dhambi kukiri kufanya maamuzi kimakosa inapotokea kwa mustakabali mwema wa mahusiano.
5.   Kuwa na hasira zisizo na mpangilio; Ni makosa makubwa kuwa na hasira zisizo na mpangilio kwa mwenzako au kuhamisha hasira kutoka ofisini au kwenye shughuli yo yote unayoifanya na kuzipeleka nyumbani.
Nyumbani ni mahali ambapo inakiwa iwe ni pakupatia faraja na pumziko stahili.
6.   Kutojishughulisha na kumuelewa mwenzako; Ni jambo jema kwa mustakabali mzuri mahusiano kufanya jitihadi kumuelewa mwenzako anakuweje katika hali ya furaha au huzuni. Hili ni muhimu sana katika mahusiano hata katika urafiki wa kawaida. Hii ni nguzo muhimu sana katika kudumisha mahusiano kwa wanandoa. Kinyume cha hapo ni kujenga mifarakano isiyo lazoma.
7.   Kutomshukuru mwenzako anapokuwa amefanya jambo zuri; Ni vizuri inapotokea mwanaume/mwanamke kafanya jambo jema kumshukuru ili kumpa moyo wa kufanya vizuri zaidi siku nyingine. Kwa mfano kama mwanaume/mwanamke ameamua kwa upendo kukununulia zaidi ya nguo ni busara kumshukuru kwanza kwa zawadi hiyo badala ya kulaumiwa kwamba nguo hiyo siyo nzuri au imeshapitwa na wakati, umeuziwa bei mbaya, karudishe nakadhalika.
Mambo yote hayo niliyoyataja hapo juu yanaweza kuepukwa, iwapo utakuwa mtafiti  na utamweka Mungu karibu  katika maisha yako yote.  Na pia kwa ushauri naomba tuwasilianae kwa barua pepe ya fkmwamoto@gmail.com  kwa ushauri makini wa masuala ya mahusiano.Tuesday, 4 April 2017

JIFUNZE MAARIFA YA KUIFANYA NDOA YAKO KUWA NA FURAHA DAIMA

Leo ningenda turudie mada ambayo tulikwishaiongelea hapa awali kuhusu tofauti za kijinsia ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa ni kiini cha migogoro ya hapa na pale katika maisha yetu ya ndoa.

Ziko tofauti nyingi za kijinsia kati ya wanawake na wanaume, ambazo mara nyingi zimekuwa chanzo cha migongano, migogoro na mivutano katika ndoa. Kutokuzifahamu tofauti hizi kumesababisha wanandoa kupeana upendo ambao kila mmoja angependa apatiwe, badala ya upendo ambao mwenzake angependa apatiwe yeye, kulingana na silika ya jinsia yake. 

Mara nyingi wanawake wamewapa wanaume malezi ya kuwajali, badala ya malezi ya kuonyesha kuwa na Imani nao. Wakati huo huo, wanaume wamewapa wanawake malezi kuonyesha kuwa na Imani nao, badala ya malezi ya kuwajali. Kutokana na mpishano huu, ndoa nyingi zimejikuta katika mivutano mingi, na changamoto ya kutokuridhishana, kwa pande zote mbili.

Utakuta, kwa vile mahitaji ya mwanamke ya msingi ya hisia za moyo ni mwenzi wake kumjali, basi anafikiri ndiyo mahitaji ya msingi ya mwanaume pia. Vivyo hivyo, utakuta mwanaume anataka mpenzi wake aonyeshe kuwa na imani naye. Hivyo, anajaribu kutoa mapenzi ya kuonyesha kuwa na Imani kwa mwenzi wake hitaji ambalo yeye angependa apatiwe na huyo mwenzi wake. Kila mmoja, pasipo kujua, anatoa aina ya mapenzi ambayo yeye angependa apatiwe, badala ya mapenzi ambayo mwenzi wake angependa apatiwe, kutokana na tofauti ya kijinsia aliyonayo.

Kwa kuelewa tofauti hizi za jinsia, na kwa kujitahidi kuuweka ufahamu huo katika matendo, misuguano iliyoko katika ndoa kati ya wanawake na wanaume itaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Ingawa hii pekee yake haitoshi kumaliza mivutano na migogoro katika ndoa, lakini ni moja ya njia muhimu ya kuboresha mahusiano katika ndoa.

Kuna wanandoa ambao, hata pasipo ufahamu huu, wameweza kuchukualiana na kuishi pamoja kwa mafanikio, na kuweza kuoanisha tofauti hizi za kijinsia. Hii ni kutokana na kipawa na alichonacho mmojawapo au wote wawili, katika kuoanisha tofauti hizi. Lakini, kufanikiwa huku pasipokuwa na ufahamu huu kunatokana  na kipawa cha kuzaliwa.

Lakini hata kama mtu anacho kipawa cha kuzaliwa, kukiboresha kupitia kuongeza ufahamu ni jambo la msingi. Hata kama ndoa ni bora, siku zote kuna nafasi ya kuzidi kuboresha zaidi na zaidi kupitia kuongeza ufahamu kuhusu ndoa. Maarifa siku zote ni silaha. Yaani maarifa yanampa mtu uwezo wa kutawala jambo.

Dr. Abraham Maslow, mwanasaikolojia mashuhuri wa karne ya ishirini, anaeleza kuhusu ufahamu na maarifa, kama ifuatavyo;
Elimu, ujuzi, ufahamu, kuijua kweli, na udhihirisho ni tiba ya hali ya juu…….na kama     ufahamu unatibu, basi kukosa ufahamu kunasababisha kuugua.

Maarifa, ufahamu, ujuzi au elimu ni silaha muhimu sana kwa binadamu, silaha ambayo ikimpa kudhibiti mambo, na kutawala changamoto mbalimbali katika maisha yake. Na katika ndoa pia, maarifa yanayohusu ndoa ni moja ya mhimili muhimu.


Sunday, 6 November 2016

MIGOGORO YA NDOA NA TOFAUTI YA KIJINSIA


Ziko tofauti nyingi za kijinsia kati ya wanawake na wanaume, ambazo mara nyingi zimekuwa chanzo cha migongano, migogoro na mivutano katika ndoa. Kutokuzifahamu tofauti hizi kumesababisha wanandoa kupeana upendo ambao kila mmoja angependa apatiwe, badala ya upendo ambao mwenzake angependa apatiwe yeye, kulingana na silika ya jinsia yake.
Mara nyingi wanawake wamewapa wanaume malezi ya kuwajali, badala ya malezi ya kuonyesha kuwa na Imani nao. Wakati huo huo, wanaume wamewapa wanawake malezi kuonyesha kuwa na Imani nao, badala ya malezi ya kuwajali. Kutokana na mpishano huu, ndoa nyingi zimejikuta katika mivutano mingi, na changamoto ya kutokuridhishana, kwa pande zote mbili.
Utakuta, kwa vile mahitaji ya mwanamke ya msingi ya hisia za moyo ni mwenzi wake kumjali, basi anafikiri ndiyo mahitaji ya msingi ya mwanaume pia. Vivyo hivyo, utakuta mwanaume anataka mpenzi wake aonyeshe kuwa na imani naye. Hivyo, anajaribu kutoa mapenzi ya kuonyesha kuwa na Imani kwa mwenzi wake hitaji ambalo yeye angependa apatiwe na huyo mwenzi wake. Kila mmoja, pasipo kujua, anatoa aina ya mapenzi ambayo yeye angependa apatiwe, badala ya mapenzi ambayo mwenzi wake angependa apatiwe, kutokana na tofauti ya kijinsia aliyonayo.
Kwa kuelewa tofauti hizi za jinsia, na kwa kujitahidi kuuweka ufahamu huo katika matendo, misuguano iliyoko katika ndoa kati ya wanawake na wanaume itaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Ingawa hii pekee yake haitoshi kumaliza mivutano na migogoro katika ndoa, lakini ni moja ya njia muhimu ya kuboresha mahusiano katika ndoa.
Kuna wanandoa ambao, hata pasipo ufahamu huu, wameweza kuchukualiana na kuishi pamoja kwa mafanikio, na kuweza kuoanisha tofauti hizi za kijinsia. Hii ni kutokana na kipawa na alichonacho mmojawapo au wote wawili, katika kuoanisha tofauti hizi. Lakini, kufanikiwa huku pasipokuwa na ufahamu huu kunatokana  na kipawa cha kuzaliwa.
Lakini hata kama mtu anacho kipawa cha kuzaliwa, kukiboresha kupitia kuongeza ufahamu ni jambo la msingi. Hata kama ndoa ni bora, siku zote kuna nafasi ya kuzidi kuboresha zaidi na zaidi kupitia kuongeza ufahamu kuhusu ndoa. Maarifa siku zote ni silaha. Yaani maarifa yanampa mtu uwezo wa kutawala jambo.
Dr. Abraham Maslow, mwanasaikolojis mashuhuri wa karne ya ishirini, anaeleza kuhusu ufahamu na maarifa, kama ifuatavyo;
Elimu, ujuzi, ufahamu, kuijua kweli, na udhihirisho ni tiba ya hali ya juu…….na kama     ufahamu unatibu, basi kukosa ufahamu kunasababisha kuugua.
Maarifa, ufahamu, ujuzi au elimu ni silaha muhimu sana kwa binadamu, silaha ambayo ikimpa kudhibiti mambo, na kutawala changamoto mbalimbali katika maisha yake. Na katika ndoa pia, maarifa yanayohusu ndoa ni moja ya mhimili muhimu.

Monday, 17 October 2016

NGUZO KUMI ZA MWANAUME BORA ALIYEOA

Habari za majukumu mbalimbali ya kiuchumi ndugu wasomaji wa blogu hii, bila shaka nyote ni wazima kwa uweza wa mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa wale ambao afya zao zimetetereka kidogo Mungu yu pamoja nanyi mtapona.
Leo napenda kutaja mambo kumi muhimu katika kudumisha mahusiano ya aina yote lakini hasa ndoa na uchumba: -
1. Mungu.
2. Upendo.
3. Roho.
4. Kujitolea
5. Agano.
6. Kukubaliana.
7. Mawasiliano.
8. Kusameheana.
9. Kujitawala.
10. Kuwa msaada kwa mwenza wako.

Ufafanuzi wa kina wa kila kipengele unapatikana kwenye blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ambayo gharama yake ya kujiunga uwanachama ni TZS. 10,000.00 kwa Airtel Money 0784190882 au TiGO pesa 0719841988. Blogu hii imeshehena makala mbalimbali kuhusiana na mbinu za kujenga na kuboresha mahusiano. Fanya uamuzi hutajutia uamuzi wa kujiunga na blogu husika.

Karibu kwenye makala ijayo na waalike na wenzio, ili uendelee kupata maarifa ya kuimalisha na kuboresha mahusiano.

Monday, 10 October 2016

MAMBO YANAYOATHIRI MALEZI YA WATOTO

Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu makala ya mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya watoto. Pia napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu kusoma makala zangu ambazo natoa kila wiki.
Katika hali inayokubali katika jamii zetu, mtoto ni matokeo ya wawili waliyokubaliana kuishi kama mke na mme baada au kabla ya kufunga ndoa. Japo mara nyingine watoto wanapatikana pasipo na lengo la kufunga ndoa. Leo niongee mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya mtoto kwa ujumla.
Makuzi ya mtoto/watoto ni jukumu la muhimu sana kwa mzazi yo yote katika jamii.

Katika tafiti mbalimbali za kisayansi makuzi anayopata mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 12 yanaakisi tabia atakayokuwa nayo katika utu uzima wake. Mambo 4 yafuatayo yanayoathiri makuzi ya mtoto ni kama yafuatavyo: -
1. Kuadibisha: Hatua za kinidhamu unazochukua dhidi ya mtoto wako huathiri malezi yake. Wataalam wa malezi ya watoto wanashauri malezi yetu yawe shirikishi kwa maana ya kwamba kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutukana watu, utoro shuleni, ugomvi n.k ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwa nini haifai kufanya jambo fulani, ili kumpatia nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo. Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali. Pia hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kusababisha hofu kwa watoto wako, ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu hata wenzao pia. Hata hivyo, pia haitakiwi kuwa mpole mno kwa sababu watoto wanaweza kuendelea kwa wakosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wao katika jamii na shuleni.
2. Mazingira: Neno mazingira kwa tafsiri fupi ni vitu vyote vinavyotuzunguka hewa, miti, majengo, watu, wanyama, shule, nyumba za ibada .n.k. Mazingira ya mtoto yanaathiri ya moja kwa moja kwa mtoto hasa ya nyumbani na shuleni. Muda mwingi wa makuzi ya watoto hutumika nyumbani na shuleni. Mtoto anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. mambo hayo uathiri moja kwa moja utazamo wa mtoto wa kimaisha. Pia mtoto ambaye anasoma shule ambayo kila saa anakosa amani kutokana na kutishiwa kupigwa na walimu au wanafunzi wenzie hujengewa hali ya kuwa na wasiwasi na kutopenda kwenda shuleni na shule.
3. Mawasiliano: Mtoto ashirikishwe katika baadhi ya maamuzi ya ki-familia kama vile masuala ya chakula, vinywaji, maongezi n.k. Ninaposema kushirikishwa katika suala ya chakula ni katika hali ya kujenga tabia ya ushirikishwaji na kumpa uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake. Pia katika maongezi nina maana mtoto sema jambo lo lote ni muhimu kumsikiliza na siyo vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele. Tabia hiyo, itamsaidia kwa kumpatie uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.
4. Malezi: Mfumo wako wa malezi unaweza kumjenga mtoto wako au kumharibu. Kuweka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo huwajengea hali ya kujisikia kuathaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo kuwaongezea furaha na amani. Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya Imani ya kupendwa imejengwe kwenye akili zao.
Kwa hiyo, wazazi tuna jukumu kubwa sana katika kujenga watoto wetu kisaikologia katika umri wa miaka 0 hadi miaka 12. Kumjenga mtoto baada ya miaka 12 na kuendelea inakuwa vigumu sana, japo inaweza kumbadilisha.
Jiunge na blog ili upate kila makala ya blog hii.


Friday, 7 October 2016

MATARAJIO YA WANANDOA KWENYE MAISHA YA NDOA

Karibuni ndugu wasomaji wa mara kwa mara wa wavuti na wale ambao ni mara ya kwanza wameingia kwenye wavuti.

Wanandoa huwa na matarajio mengi sana katika maisha yao ya ndoa hasa matarajio mazuri daima.  Maisha ya ndoa ni mchakato ambao hupita katika hatua kuu nne (4) yaani; kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Lakini si ndoa zote hupitia hatua hizo zote nne (4) baadhi hupitia hatua tatu (3) au mbili (2) kutokana na baadhi ya wanandoa kuacha kumkabidhi mlezi na mwanzilishi wa ndoa duniani yaani; Mungu. Kwenye makala hii, sitaki kuongelea sababu anuai zinazosababisha baadhi ya ndoa kutopitia hatua kuu nne (4) mzunguko wa maisha ya ndoa. Baadhi ya matarajio maisha ya iliyo katika hatua ya pili (2) ni kama yafuatavyo:-

ü  Changamoto za masuala ya kifedha.

ü  Changamoto za kimawasiliano baina yao.

ü  Changamoto zinazoletwa na wanandugu na watoto.

ü  Upweke.

ü  Kukua/kudumaa kiroho.

ü  Migogoro.

ü  Magonjwa.

Kipengere cha 4 hadi 7 nitavifafanua lakini cha 1 hadi 3 zilishavifanunua kwenye makala zangu za awali za changangamoto zinazosababishwa na wanandoa wenyewe na changamoto zinazosababishwa watu wengine wasiyowanandoa.

Upweke; Kutokana na kuongezeka kwa majukumu na uwajibikaji kwa masuala ya kifamilia maisha uliyokuwa unategemea kuwa yatakuwa daima ya amani na furaha huanza kubadilika na hapo ndipo hali ya kutaka kukaa kiupweke uanza kujitokeza ili kutafari zaidi majukumu ya kifamilia na hamu ya tendo la ndoa hupungua kwa sababu ubongo unakuwa umezingirwa na mawazo ya namna ya kutatua majukumu yaliyo mbele kama vile ada, kodi ya nyumba, gharama za usafiri kwenda na kurudi kazini, chakula nakadhalika.

Migogoro; Kutokana ndoa kuwa katika hatua ya kukua  tabia zote zilizokuwa zimevichwa na wanandoa wote uanza kudhihirika kwa sababu tabia haiwezi kufichwa daima. Tabia za kiburi, jeuri, dharau, hasira, uasherati nakadhalika uanza kuonekana na kuleta migogoro ya hapo pale katika ndoa. Hatua hii inahitaji busara na hekima kubwa hasa kwa kumshirikisha Mungu, ili kuweza kuivuka na ndoa nyingi sana huishia hatua hii.

Magonjwa; Kwa sababu za kimazingira na vyakula imekuwa ni jambo la kawaida kwa binadamu kuugua kwa muda mrefu au mfupi. Inapotokea uuguaji ni wa muda mrefu jambo ili uyumbisha sana hali ya uchumi wa wanandoa na kama hakuna upendo wa dhati basi hata misingi ya ndoa uanza kulegalega.

Mwacheni Mungu awe mtawala katika maisha yenu ya ndoa kwa maana yeye ndie muasisi ya taasisi ya ndoa hakika ndoa yenu itadumu na itakuwa kisima cha amani na furaha. Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com bure.

Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.

 

 

 

 

 

Saturday, 10 September 2016

JE, UNATAKA KUWEKEZA?


Je,unahitaji kuwa mwekezaji katika biashara ambayo haitakulazimu kuacha kazi yako ya sasa au masomo yako?. Kama jibu lako ni ndio ,basi fursa hii yaweza kuwa ndiyo ambayo umekuwa ukiingojea.

HELPING HANDS INTERNATIONAL (H2i)
Hili ni Shirika lisilo la kiserikali lenye makao Makuu nchini Ufilipino kwa kazi kubwa ya kuwasaidia watu masikini,walemavu,yatima wajane na wenye magonjwa sugu nao kuishi maisha ambayo Mungu anapenda. Unaweza kutembelea tovuti hii kwa taarifa zaidi.


https://helpinghandsinternational.biz/how-it-works.php

Hivyo H2i imekuwa ikifanya hivyo ili kusaidia makundi haya duniani kote bila kubagua rangi dini wala kabila.
Shirika hili la H2i linamhusu yule tu anayeguswa na mahitajj ya hayo makundi na anayependa fedha zake zitumike kusaidia wahitaji .


WADHAMINI WA HELPING HANDS INTERNATIONAL.

Helping Hands international linafanya kazi kwa kudhaminiwa na makampuni makubwa duniani kama:
1) Hyundai motors
2) HP
3) Apple
4) Glo line
5) Diamond Bank
6)Bill Gate Foundation
7)Gac motors
8)LG(Life's Good)


FAIDA YA KUWA BALOZI WA H2i

Fursa hii inakupatia kipato kikubwa na endelevu na Shirika linakupa bonas nyingine kama:
1. Kupewa iPad
2. Kupewa laptop
3. Kupewa magari 2
4. Safari za kimataifa
5. Kusomeshewa watoto wako.
6. Kupewa mikopo isiyo na riba.
7. Kupewa nyumba ya kifahari.
8. Kusomesha watoto yatima kutoka kijijini kwako.
9. Kupewa mafunzo ya kiuongozi na biashara nje ya nchi.
10. Kulipwa fedha kila mwaka tofauti na bonus.


JINSI YA KUWA MWANACHAMA

Ili uwe Mwanachama unatakiwa kutoa mchango (hisa 1=$40)sawa na Tsh 90000/= unaweza kununua hisa nyingi kadri uwezavyo na unakuwa balozi wa H2i wa milele bila kufutwa,na unafanya donation ya $40 mara moja maisha yako yote.

JE, MWANACHAMA ATAUZA BIDHAA GANI ILI ALIPWE?

Mwanachama hauzi bidhaa kabisa kwa kuwa shirika halina bidhaa yoyote ya kuuza ila linatoa huduma tu.
Mwanachama anapojiunga anafanya kazi moja tu kubwa, kuwashirikisha watu wengine wawili kujiunga na shirika hili nao watapaswa kushirikisha watu wawili wawili na mtandao wako utaendelea kukualika,na kwa kila mtu atakayejiunga kutokana na wewe shirika litakulipa $8 kwa mtu mmoja.


Shirika pia linakuruhusu kutengeneza Mabalozi wengine wengi na kuanza kupokea Dola 8 kila unapomsajili balozi mpya. Aidha, Kila mtu anayejiunga kuwa balozi wa Shirika anatakiwa kuhakikisha anatafuta watu 2 ambao nao watakubali kujiunga na Shirika na kushiriki fursa hii adhimu.

H2i ina mfumo wa 2 by 2 matrix unaowezesha kila balozi kupanda ngazi hatua kwa hatua. Kuna ngazi 5 ambazo kila moja ina zawadi (bonus) inayotolewa kwa kila anayeingia ktk ngazi husika. Kila mtu anaweza
kupanda ngazi kuanzia daraja la kwanza hadi daraja la Tano. Zawadi zitolewazo ni kama iluvyoorodheshwa hapo juu. (Ipad, Laptop, gari jipya, mkopo usio na riba, kusomeshewa watoto 2, kupendekeza wahitaji 2 watakaosaidiwa na Shirika pamoja na kupata fursa za kusoma na kufanya ziara za kimataifa.


KUMBUKA, Huu sio UPATU,kwamba utakapojiunga tu unakaa na kusubiri kulipwa na kupewa zawadi, kuna wajibu utakaopaswa kutimiza, wajibu wako ni kushirikisha watu wengine na kuwaelekeza inapobidi .

Huhitaji kuacha kazi yako ya awali ili ufanye kazi na asasi hii. Karibu nitakuelekeza na kukusimamia hadi mwisho.

Kwa maelezo zaidi napatikana whatsapp 0784190882 au nipigie 0767572442/0719841988