Thursday 5 April 2018

MIGOGORO KATIKA NDOA NA MAHUSIANO


Kama nilivyoeleza kwenye makala yangu ya changamoto zinazosababishwa nawanadoa wenyewe mmojawapo ni mawasiliano(kutokuelewana). Hii ndio changamoto kubwa sana katika ndoa na ndio chanzo cha taraka nyingi kwa mujibu takwimu za kimataifa. Kwa bahati mbaya tarakwimu za hapa kwetu nimeshindwa kuzipata kwa njia ya vyanzo rasmi vya vinavyohusika na takwimu.


Kimsingi ni kwamba migogoro inayosababishwa na kutoelewana chanzo chake kinaweza kuwa ni mmoja wa wanadoa au wote wawili. Migogoro kikawaida ipo kwenye ndoa zote ila hutofautiana kwa kiwango. Ipo kwenye kila ndoa kutokana na sababu za malezi na tabia za asili za wanandoa. Na kawaida migogoro ukua kutokana na kukosa utayari wa kuitatua kwa wanandoa wenyewe ama kwa wote wawili au mmoja wao. Inapotokea hakuna utayari kwa wote wawili, ndoa haiwezi kudumu na kama ni kwa mmoja wao tu kuna asilimia fulani ndoa kuweza kudumu na kama wote wako tayari kutatua ndoa hii inakuwa na asilimia 100 kudumu.


Kama nilivyoongea kwenye makala tajwa hapo juu. Migogoro ya kutoelewana ipo inayotokana na mahitaji ya kawaida na ya kimwili. Leo tutaongelea migogoro inayotokana na mahitaji ya kawaida ya kimwili. Ninavyosema mahitaji ya kawaida nina maana mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, mavazi na mahitaji mengine ambayo siyo msingi yaani; mahitaji ya kumpendezesha mwanandoa, kushaurishwa, kuthaminiwa n.k.


NAMNA YA KUPAMBANA NA MIGOGORO INAYOTOKANA NA MAHITAJI YA KAWAIDA


1.    Kuwa mkweli kuhusu hali ya kipato chake.


Kuwa mkweli wa hali yako ki-uchumi yaani; kuwa mkweli kwa mwenza wako kuhusu hali ya mapato yako. Na ukweli huu ni vizuri ufanyike kabla ya kufunga ndoa. Ni vizuri sana kama utauvaa uhalisia wako kipato kipindi chote cha uchumba. Hili, ni muhimu sana kwa sababu nitakusaidia kujua kama mchumba wako ni wa kiwango chako au la. Ukidanganya katika suala hili unakuwa umepande mgogoro ambayo itakuwa vigumu kuusuluhisha na unakuwa umejenga hali ya kutoaminika.


2.    Onyesha kujali hitaji la mwenza wako.


Jitahidi kujali mahitaji ya mwenza wako kwa kumtimizia hitaji lake kama uwezo unaruhusu na kama unaona sihitaji la msingi, tafuta lugha nzuri ya kumweleza ni kwa nini unaona hitaji lisitimizwe na bila kuonyesha dalili za kupuuza au kuonyesha sihitaji la msingi.


3.    Epuka kuonyesha upendeleo katika kusaidia ndugu.


Katika familia zetu za ki-afrika kuna matatizo ya kila namna kwenye familia zetu yaani; kwa upande wa mke na mwanaume. Inapotokea kuna mahitaji upande wa familia za upande mmojawapo ni muhimu sana kuweka uwiano wa misaada inayotolea, ili kuepuka kuonyesha upendeleo.


4.    Epuka kuonyesha upendeleo kwa wageni wanao watembelea nyumbani.

Ni jambo la kawaida sana ndugu wa pande zote kutamani kuwatembelea wanandoa katika hali ya amani au matatizo. Ni vizuri kujitahidi kutoonyesha unyanyapaa kwa wanandugu wa upande mmoja hali hii inaweza kuleta mgogoro mkuu.


5.    Epuka kuonyesha dharau dhidi ya mila na desturi za mwenza wako.


Inapotokea wanandoa ni makabila tofauti ina maana watakuwa wamekulia kataika mila na desturi tofauti. Mila na desturi uhusisha namna ya kuongea, mapishi, tofauti za ki-maendeleo baina ya kabila moja na nyingine. Si vizuri kuonyesha dharau hata kama ni katika hali ya utani kwa sababu hiyo huonyesha hisia zako dhidi ya mwenzako hata kama utasema unamtania.


6.    Epuka utani unaoeleka kweli uhalisia kimaumbile.


Jitahidi kuepuka utani unaohusiana na maumbile kama vile watu wafupi au wanene wana kasoro 1,2,3 n.k. wakati ukijua kwamba mwenza wako nao ana maumbile kama hayo. Utani kama huo hufanya mtaniwa kujisikia vibaya na kuleta migogoro katika ndoa.


7.    Kushaurishwa katika mambo ya msingi ki-familia.


Kitabia kila binadamu anapenda kuthaminiwa katika mambo tofauti tofauti kama kazi zake, ushauri n.k. Katika mambo ya msingi ya maendeleo ya kifamilia kama vile ununuzi wa kitu cho chote cha kifamilia kama vile samani, na vitu vingine muhimu katika maisha yetu ya kila siku.


Ili kuendelea kupata makala hizi weka jina lako na barua pepe kwenye kisanduku kidogo mkono wa kulia. 


No comments:

Post a Comment