Monday 30 June 2014

MAMBO 4 YANAYOATHIRI MAKUZI YA WATOTO

Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu makala ya mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya watoto. Pia napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu kusoma makala zangu ambazo natoa kila wiki.
Katika hali inayokubali katika jamii zetu, mtoto ni matokeo ya wawili waliyokubaliana kuishi kama mke na mme baada au kabla ya kufunga ndoa. Japo mara nyingine watoto wanapatikana pasipo na lengo la kufunga ndoa. Leo niongee mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya mtoto kwa ujumla.
Makuzi ya mtoto/watoto ni jukumu la muhimu sana kwa mzazi yo yote katika jamii.

Katika tafiti mbalimbali za kisayansi makuzi anayopata mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 12 yanaakisi tabia atakayokuwa nayo katika utu uzima wake. Mambo 4 yafuatayo yanayoathiri makuzi ya mtoto ni kama yafuatavyo: -
1. Kuadibisha: Hatua za kinidhamu unazochukua dhidi ya mtoto wako huathiri malezi yake. Wataalam wa malezi ya watoto wanashauri malezi yetu yawe shirikishi kwa maana ya kwamba kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutukana watu, utoro shuleni, ugomvi n.k ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwa nini haifai kufanya jambo fulani, ili kumpatia nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo. Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali. Pia hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kusababisha hofu kwa watoto wako, ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu hata wenzao pia.  Hata hivyo, pia haitakiwi kuwa mpole mno kwa sababu watoto wanaweza kuendelea kwa wakosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wao katika jamii na shuleni.
2. Mazingira: Neno mazingira kwa tafsiri fupi ni vitu vyote vinavyotuzunguka hewa, miti, majengo, watu, wanyama, shule, nyumba za ibada .n.k. Mazingira ya mtoto yanaathiri ya moja kwa moja kwa mtoto hasa ya nyumbani na shuleni. Muda mwingi wa makuzi ya watoto hutumika nyumbani na shuleni. Mtoto anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. mambo hayo uathiri moja kwa moja utazamo wa mtoto wa kimaisha. Pia mtoto ambaye anasoma shule ambayo kila saa anakosa amani kutokana na kutishiwa kupigwa na walimu au wanafunzi wenzie hujengewa hali ya kuwa na wasiwasi na kutopenda kwenda shuleni na shule.
3. Mawasiliano: Mtoto ashirikishwe katika baadhi ya maamuzi ya ki-familia kama vile masuala ya chakula, vinywaji, maongezi n.k. Ninaposema kushirikishwa katika suala ya chakula ni katika hali ya kujenga tabia ya ushirikishwaji na kumpa uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake. Pia katika maongezi nina maana mtoto sema jambo lo lote ni muhimu kumsikiliza na siyo vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele. Tabia hiyo, itamsaidia kwa kumpatie uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.
4. Malezi:  Mfumo wako wa malezi unaweza kumjenga mtoto wako au kumharibu. Kuweka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo huwajengea hali ya kujisikia kuathaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo  kuwaongezea furaha na amani. Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya Imani ya kupendwa imejengwe kwenye akili zao.
Kwa hiyo, wazazi tuna jukumu kubwa sana katika kujenga watoto wetu kisaikologia katika umri wa miaka 0 hadi miaka 12. Kumjenga mtoto baada ya miaka 12 na kuendelea inakuwa vigumu sana, japo inaweza kumbadilisha.
Jiunge na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ili UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO YA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA. Maoni na ushauri mbalimbali yanakaribishwa. Karibu PAMOJA TUSONGE MBELE.


Monday 23 June 2014

MAKOSA SABA (7) YANAYOFANYWA NA WANANDOA MENGI

Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu baadhi ya makosa ambayo hufanywa na wanandoa wengi. Pia napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu kusoma makala zangu ambazo huwa natoa kila wiki.
Leo nitaongelea makosa saba (7) ambayo mara nyinyi hufanywa na wanandoa na kusababisha kuibuka kwa migogoro katika mahusiano. Makosa hayo ni kama yafuatavyo: -
1.   Kususia tendo la ndoa bila sababu ya msingi; Tendo la ndoa ni mmojawapo wa nguzo muhimu ya ndoa zote. Kwa hiyo, inapotokea mmoja wa wanandoa kuamua kumnyima mwenzake tendo la ndoa bila sababu ya msingi ni tendo ambalo linaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa bila kujali ni ya kidini, kimila au kiserikali.
2.   Kumsema vibaya mwenzako wako kwa rafiki/ndugu; Ni makosa makubwa sana kwa mustakabali wa ndoa kwa mmoja wa wanandoa kumsema vibaya mwenzake kwa rafiki zake au ndugu zake badala ya kumuelimisha ili kuondoa  kasoro unazoziona kwake.
3.   Kutotimiza yale unayosema; Ni kosa kubwa sana kwa mwanandoa kutotimiza/kutenda yale anayoahidi kwa mkewe/mmewe bila sababu ya msingi. Katika mahusiano hutokea misukosuko ya hapa na pale na nyingi hutokea mmoja wa wanandoa kuomba msamaha na kukiri kutorudia vitendo fulani ambavyo ni kero kwa mwenzako kwa mfano; kulala nje, kuchelewa kurudi nyumbani bila taarifa yo yote, nakadhalika.
4.   Kutokukubali makosa; Ni busara kwa mstakabali mzuri wa ndoa kukubali makosa inapotokea kuwa mmoja wa wanandoa kafanya makosa. Imekuwa ni vigumu sana kwa wanandoa hasa wanaume kukubali makosa inapotokea wamefanya makosa na badala yake huonyesha kukiri kwa vitendo yaani; kufuata mapendekezo ya wake zao na siyo kukubali kwamba maamuzi yao ya awali yalikuwa na makosa. Si dhambi kukiri kufanya maamuzi kimakosa inapotokea kwa mustakabali mwema wa mahusiano.
5.   Kuwa na hasira zisizo na mpangilio; Ni makosa makubwa kuwa na hasira zisizo na mpangilio kwa mwenzako au kuhamisha hasira kutoka ofisini au kwenye shughuli yo yote unayoifanya na kuzipeleka nyumbani.
Nyumbani ni mahali ambapo inakiwa iwe ni pakupatia faraja na pumziko stahili.
6.   Kutojishughulisha na kumuelewa mwenzako; Ni jambo jema kwa mustakabali mzuri mahusiano kufanya jitihadi kumuelewa mwenzako anakuweje katika hali ya furaha au huzuni. Hili ni muhimu sana katika mahusiano hata katika urafiki wa kawaida. Hii ni nguzo muhimu sana katika kudumisha mahusiano kwa wanandoa. Kinyume cha hapo ni kujenga mifarakano isiyo lazoma.
7.   Kutomshukuru mwenzako anapokuwa amefanya jambo zuri; Ni vizuri inapotokea mwanaume/mwanamke kafanya jambo jema kumshukuru ili kumpa moyo wa kufanya vizuri zaidi siku nyingine. Kwa mfano kama mwanaume/mwanamke ameamua kwa upendo kukununulia zaidi ya nguo ni busara kumshukuru kwanza kwa zawadi hiyo badala ya kulaumiwa kwamba nguo hiyo siyo nzuri au imeshapitwa na wakati, umeuziwa bei mbaya, karudishe nakadhalika.
Mambo yote hayo niliyoyataja hapo juu yanaweza kuepukwa,  iwapo utakuwa mtafiti  na utamweka Mungukaribu  katika maisha yako yote.  Na pia nakushauri kujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala za ushauri makini wa masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


 

Friday 20 June 2014

UNAPOINGIA KWENYE NDOA JIANDAE PIA NA YATOKANAYO NA NDOA

Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kumshukuru mwenye Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii adimu ya kuwaandikieni makala hii fupi. Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji  wangu wapendwa kwa kuendelea kunitia moyo kwa ushauri na maoni yenu mazuri, naomba muendelee na moyo nawaombeni muwaalike na marafiki zenu kusoma makala za blogu hii.
Leo hii napenda kuongelea sababu za ndoa nyingi kuwa na migogoro inayoishia kuachana. Tafiti nyingi sana zinaonyesha kwamba wastani wa  ndoa 65% zina migogoro mingi ambayo inaweza kuepukika kwa kupata ushauri muafaka. Takwimu hiyo ni kwa mujibu wa tarakwimu kwenye nchi zilizoendea na zinazoendelea. Baadhi ya sababu za ndoa nyingi kuingia katika matatizo ni kama zifuatazo: -

1.    Wanandoa wengi wanaingia kwenye ndoa na mtazamo wa kwamba ndoa ni raha tupu; Wanaume/wasichana wengi wamekuwa wakiingia kwenye ndoa na mtazamo wa kwamba maisha ya ndoa ni raha tupu kama inavyokuwa wakati wa uchumba. Yaani tabia za kiuchumba kama vile kwenda kula Hoteli, kutoka (outing), kutumia takeaway nakadhalika badala ya kupika. Kwa sababu ya huo mtazamo finyu,  wanandoa wengi  wanakuwa hawajajiandaa kisaikologia kukabiliana na migogoro. Kwa hiyo, migogoro midogo midogo kama vile kuambiwa hakuna hela ya kufanya starehe ndogo ndogo za kimazoea ya kiuchumba zinapoanza kujitokeza katika ndoa, mmoja wa wanandoa  huishia kuchanganyikiwa na kuhisi kusalitiwa na wenzi wao. Kutokana na hisia hizo hasi  mawazo ya kujiamini  dhidi ya hisia hizo husababisha nyumba kuanza kuyumba. Kwa sababu ya hisia  hizo hasi mawasiliano ya kawaida kama wanandoa huingia kasoro.
2.    Wanandoa wengi huingia kwenye ndoa kwa tamaa ya mali; Ni ukweli uliyo wazi kwamba kuna wanaume/wasichana wengi huingia katika mahusiano na hatimaye ndoa kwa tamaa tu ya mali za mmoja wa mwanandoa. Ndoa kama hii, mhimili wake unakuwa ni mali za mmoja wa wanandoa kwa hiyo, inapotokea kwamba hizo mali zimeisha ndoa huanza kuteteleka au kuanguka.
3.    Tendo la ndoa; Wanandoa wengi huingia kwenye ndoa wakiwa na imani kwamba watafanya tendo la ndoa kila siku na mara kadhaa kwa siku.  Inapotokea mmoja wa wanandoa hapendi utaratibu wa kufanya tendo la ndoa kwa utaratibu huo,basi  hili nalo huwa chanzo cha kuitilafiana. Iwapo wanandoa wana  mtazamo unaofafana basi hilo haliwi tatizo na mmojawapo akiwa kinyume chake inakuwa  ni chanzo cha mgogoro. Hili ni mojawapo wa sababu kubwa inayoleta matatizo katika ndoa nyingi. Kimsingi ni kwamba binadamu tunatofautiana  sana katika uhitaji wa tendo la ndoa. Kwenye suala hili ni vizuri kufahamiana vema kimwili, ili kudumisha mstakabali ya ndoa. Hoja ya tendo la ndoa ni changamoto kubwa sana katika ndoa hasa kama wanandoa si wa wazi. Yaani hawako tayari kuongelea masuala yanayohusiana na tendo la ndoa kiuwazi.
4.    Kutokuwa na imani ya dini; Ni ukweli usiyojificha  kwamba imani zote za kidini zinatufundisha kuvumiliana na kusameheana na kumkubali kila binadamu kwa namna alivyo na huu ndio msingi mkuu wa imani zote.Yaani mpende kila binadamu kwa namna alivyo.  Kwa maana hiyo, wanandoa wanaoishi pasipo na kumshirikisha Mungu ni rahisi sana kuingia katika migogoro kutokana na migogoro isiyo na msingi.
5.    Kuigiza tabia na uchumi; Baadhi ya wanandoa huigiza tabia na hali za kiuchumi tofauti na uhalisia wao, ili tu, waweze kuwapata watu wanao watamani kuwa wenzi wao.  Ninaposema kuigiza tabia nina maana kujifanya mpole, mchaa Mungu, mkarimu nakadhalika wakati kiuhalisia hauko hivyo. Ninaposema kuigiza kiuchumi nina maana kujifanya una uwezo wa kiuchumi na yaani; pesa kwako siyo tatizo una miradi, majumba, magari nakadhalika wakati huna kitu. Tabia hii ya kuigiza ni haifai kwa sababu mwenza wako anapogundua kwamba ulikuwa una mdanganya ndoa itakuwa imeingia hitilafu kubwa.
Mambo yote hayo niliyoyataja hapo juu yanaweza kuepukwa,  iwapo utakuwa mtafiti  na utamshirikisha Mungu katika mipango yako ya kuingia kwenye ndoa.  Na pia nakushauri kujiunga na blogu  ya  http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com  kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala za ushauri makini wa masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


Monday 9 June 2014

MANENO/TABIA 7 HATARISHI KWA HUSTAWI WA MAHUSIANO

Ndugu msomaji leo napenda niongelee maneno/tabia ambayo ni hatarishi kwa wanamahusiano (wanandoa au wachumba). Maneno hayo kwenye mabano nilishayatatolea tafsiri isiyo rasmi kwenye makala yangu ya utambulisho wa blogu. Kabla sijaenda mbali naomba leo niwape tafsiri ya ndoa kwa mujibu wa mtaalamu  wa mambo ya ndoa Ndugu Nancy Van Pelt katika kitabu chake kiitwacho “To have and to hold” “A guide to successful marriage”. Katika kitabu hiki ndoa imetafsiriwa kwamba ni  muunganiko wa upendo wa mwanamke na mwanaume katika nyanja zote za maisha na kwamba munganiko huu ni wa kimwili, kihisia, kiakili na kiroho na kwamba taasisi hii ni ya siku nyingi sawa na uwepo wa binadamu katika sayari hii.
Katika mahusiano kuna baadhi ya maneno hayafai kumwambia mwenza kwa sababu mara nyingi yameokana kuvuruga mahusiano mengi sana. Baadhi ya tabia/maneno hatarishi ni kama zifuatavyo:-
1.       Kumwambie mwanza wako wewe hujui Kitu; Neno ili kwa ujumla halifai kulitumia kumwambia mwenza wako kwa sababu tafsiri yake ni pana sana na huibua hisia nyingi sana kwa aliyeambiwa. Mara nyingi mwambiwa hujisikia kwamba hajui mambo ya unyumba. Kwa hiyo, kumuondolea unyonge ni busara ukatoa ufafanuzi ni mambo gani unaona mwenza wako hajui, na unafanyaje kumrekebisha kama mwenza wako.
2.       Kumsifia mwanamke/mwanaume mwingine; Jitahidi sana kuepuka tabia ya kumsifia mwanamke/mwanaume yo yote kimapana, hii itakuletea matatizo makubwa katika mahusiano yenu kwa sababu wa wivu ambao mara nyingi utawala mahusiano.
3.       Maneno yakudhihaki maisha ya nyumbani kwa mwenza; Maneno ya kudharau familia ya mwenza wako ki-uchumi, ki-utamaduni, ki-desturi nakadhalika.
4.       Utani dhidi ya mwenza unaogusia maumbile yake halisi; Ninaposema maumbile ninamaanisha ufupi, unene, wembamba, nakadhalika. Utani wo wote wenye kuonyesha dhihaka dhidi ya tabia zinazoenda na maumbile haya zinaweza kuleta matatizo makubwa kwenye mahusiano. Maneno kama watu wafupi Bwana, watu wanene Bwana nakadhalika. Kwa sababu suala la maumbile halina uchaguzi Mungu ndie anayepanga.
5.       Lawana za mara kwa mara dhidi ya mwenza wako; Kwa asili kila binadamu hupenda kusifiwa pale anapofanya jambo zuri na kusahihishwa si kulaumiwa pale anapokosewa. Si vizuri kulaumu mwenza wako anapokuwa amefanya jambo/kitu ambacho kwako wewe mpokeaji hakijakufuraha. Tafuta lugha nzuri ya kumweleza mwenza wako pale anapokuwa amekosea ki-mapishi, zawadi, manunuzi yo yote ya kifamilia, usafi wa nyumba, nakadhalika, tabia kama hiyo ukatisha tamaa.
6.       Kutoa siri za ndani nje; Ndoa ni mchakato na kuna mambo mengi ambayo wanandoa wanatakiwa kuelimishana ili ndoa iweze kuendeleakustawi na kudumu. Katika mambo ambayo wanandoa hawapaswi kutoa nje ni pamoja na mambo yanahusu unyumba. Ni jambo la hatari sana kwa mwanandoa kutoa siri za masuala ya unyumba kwa sababu tabia hii mara nyingi huishia kubomoa nyumba. Siri hii, haifai kutolewa nje iwe ni kumsifia au kumlaumu mwenza kuhusiana na suala la unyumba sio vizuri kwa mstakabali wa ndoa.
7.       Kuzaa nje ya ndoa; Ni dhairi kwamba wanandoa wengi wanatoka nje ya ndoa kinyume na agano la ndoa na pia maagizo ya Mungu takwimu zinaonyesha 55% ya wanandoa wanatoka nje. Taarifa hii, ni kwa mujibu wa takwimu mbalimbali za tafiti katika nchi mbalimbali duniani. Pamoja na ukweli kitendo cha mwanandoa kuzaa nje ya ndoa akiwa ndani ya ndoa ni jambo ambalo linaweza kuvunja ndoa bila kujali ni nani kafanya hivyo yaani; mme au mke.

Ili kupata maarifa ya kukabiliana na changamoto za mahusiano na kupata maarifa ya kustawisha na kudumisha mahusiano yako jiunge na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kwa kupitia kwenye airtel 0784190882 au Tigo pesa 0719841988.

Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.


Monday 2 June 2014

DALILI ZA MAHUSIANO YANAYOENDA MRAMA

Napenda kuchukua nafasi hii, kuwashukuru wale wote walitoa maoni na ushauri mbalimbali kuhusiana na makala zilizotangulia.
Jambo lo lote kabla halijatokea kunakuwa na dalili au ishara fulani za kuonyesha kutokea suala fulani. Kwa mfano kuna msemo uliyozooleka wa kwamba dalili za mvua ni mawingu ipo na misemo mingine inayofanana kama hiyo katika jamii. Katika suala la mahusiano hasa yaliyofikia hatua ya ndoa kuna dalili huwa zinajitokeza kuonyesha kwamba hali si shwari au inaelekea mwisho. Katika hali ya kawaida ya maisha yo yote kunakuwa na mzunguko huu; kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Pia katika mahusiano kuna yanayopita hatua zote hizo nne (4) na nyingine hupitia hatua tatu (3) au mbili (2) tu.
Leo naongelea mahusiano ambayo yamefikia hatua ya pili (2) yaani; kukua. Dalili za kuonyesha kwamba mahusiano yanaenda mrama kwa mujibu wa tafiti mbalimbali  ni kama zifuatazo: -
1.       Ugomvi wa mara kwa mara wa bila sababu ya msingi; Ugomvi wa mara kwa mara unaotokana na sababu zisizo za msingi ni dalili ya mahusiano yanayo kwenda mrama. Ugomvi unaweza ukasababishwa na chakula, watoto, nguo nakadhalika. Na mara nyingi sababu zinakuwa siyo hiyo inayoongelewa,  bali ni kutokana na maalimbikizo ya makosa fulani madogo ya hapo nyuma au mmoja wa wanamahusiano amepata mtu anayempotosha/kumdanganya.
2.       Dharau za kupitiza na kejeli za hapa na pale; Maneno ya dharau mpaka matusi huanza kujitokeza kwa wanahusiano ki waziwazi, ilimradi tu kuonyesha kwamba uhusiano una kwenda mrama. Maneno kama vile wewe si cho chote, ningekujua ni singeolewa na wewe, kulala nje,kuondoka nyumbani bila taarifa, kurudi usiku wa manane bila taarifa yo yote kwa mwenza, kutukana ndugu wa upande wa mwenza, kunyimwa unyumba, niko hapa kwa ajili ya watoto tu  n.k.
3.       Kuomba kuungwa mkono na watoto/wanandugu kwenye ugomvi; Tabia ya wanahusiano kuingiza watoto/wandugu kwenye ugomvi kwa kusema mwenza ndie chanzo cha ugomvi. Hii inaambatana na kutoa siri za ndani za mwenza kwa watoto/wanandugu n.k.
4.       Kuhama chumba; Kutokana na uhasama kuwa mkubwa kuamiana kuondoka kwa visngizo mbalimbali wanamahusiano hufikia hatua ya kulala vyumba tofauti. Hutokea  mwanzilishi wa ugomvi uamua kuhamia sebuleni kama vyumba ni vichache au chumba cha watoto.
5.       Madai ya kuachana ;Baada ya hatua hizo hapo juu hatua inayofuata ni ya kudai kuachana au kwenda kanisani/msikitini kueleza matatizo yao ya mahusiano. Suluhu za wachungaji na masheikh  mahusiano yanapofikia hatua hii, mara nyingi hazizai matunda. Mwanzilishi wa ugomvi uamua kwenda mahakamani kudai taraka upande serikali.
Mahusiano yanapofikia hatua ya tano (5) kama mmefunga ndoa ni vizuri kutafuta kiini cha matatizo hayo na kupiga magoti na kuomba Mungu aingilia kati kwa kuondoa ibilisi kati yenu. Pia kwa kusoma  makala za ushauri wa migogoro ya mahusiano kwenye blogu ya http://mkombozi-mahusiano unaweza kupata suluhisho kwa kuwa mwanachama.  Ada ya uanachama wa blogu tajwa hapo juu ni TZS. 10,000.00 na unailipia kwenye TiGO pesa ya 0719841988 au airtel money 0784190882 baada ya kulipa tuma e-mail address yako ya google kwenye namba yo yote kati ya hizo. Kama huna e-mail address ya google tunakushauri ufungue e-mail address husika.
 Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.