Monday 17 October 2016

NGUZO KUMI ZA MWANAUME BORA ALIYEOA

Habari za majukumu mbalimbali ya kiuchumi ndugu wasomaji wa blogu hii, bila shaka nyote ni wazima kwa uweza wa mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa wale ambao afya zao zimetetereka kidogo Mungu yu pamoja nanyi mtapona.
Leo napenda kutaja mambo kumi muhimu katika kudumisha mahusiano ya aina yote lakini hasa ndoa na uchumba: -
1. Mungu.
2. Upendo.
3. Roho.
4. Kujitolea
5. Agano.
6. Kukubaliana.
7. Mawasiliano.
8. Kusameheana.
9. Kujitawala.
10. Kuwa msaada kwa mwenza wako.

Ufafanuzi wa kina wa kila kipengele unapatikana kwenye blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ambayo gharama yake ya kujiunga uwanachama ni TZS. 10,000.00 kwa Airtel Money 0784190882 au TiGO pesa 0719841988. Blogu hii imeshehena makala mbalimbali kuhusiana na mbinu za kujenga na kuboresha mahusiano. Fanya uamuzi hutajutia uamuzi wa kujiunga na blogu husika.

Karibu kwenye makala ijayo na waalike na wenzio, ili uendelee kupata maarifa ya kuimalisha na kuboresha mahusiano.

Monday 10 October 2016

MAMBO YANAYOATHIRI MALEZI YA WATOTO

Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu makala ya mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya watoto. Pia napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu kusoma makala zangu ambazo natoa kila wiki.
Katika hali inayokubali katika jamii zetu, mtoto ni matokeo ya wawili waliyokubaliana kuishi kama mke na mme baada au kabla ya kufunga ndoa. Japo mara nyingine watoto wanapatikana pasipo na lengo la kufunga ndoa. Leo niongee mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya mtoto kwa ujumla.
Makuzi ya mtoto/watoto ni jukumu la muhimu sana kwa mzazi yo yote katika jamii.

Katika tafiti mbalimbali za kisayansi makuzi anayopata mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 12 yanaakisi tabia atakayokuwa nayo katika utu uzima wake. Mambo 4 yafuatayo yanayoathiri makuzi ya mtoto ni kama yafuatavyo: -
1. Kuadibisha: Hatua za kinidhamu unazochukua dhidi ya mtoto wako huathiri malezi yake. Wataalam wa malezi ya watoto wanashauri malezi yetu yawe shirikishi kwa maana ya kwamba kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutukana watu, utoro shuleni, ugomvi n.k ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwa nini haifai kufanya jambo fulani, ili kumpatia nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo. Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali. Pia hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kusababisha hofu kwa watoto wako, ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu hata wenzao pia. Hata hivyo, pia haitakiwi kuwa mpole mno kwa sababu watoto wanaweza kuendelea kwa wakosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wao katika jamii na shuleni.
2. Mazingira: Neno mazingira kwa tafsiri fupi ni vitu vyote vinavyotuzunguka hewa, miti, majengo, watu, wanyama, shule, nyumba za ibada .n.k. Mazingira ya mtoto yanaathiri ya moja kwa moja kwa mtoto hasa ya nyumbani na shuleni. Muda mwingi wa makuzi ya watoto hutumika nyumbani na shuleni. Mtoto anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. mambo hayo uathiri moja kwa moja utazamo wa mtoto wa kimaisha. Pia mtoto ambaye anasoma shule ambayo kila saa anakosa amani kutokana na kutishiwa kupigwa na walimu au wanafunzi wenzie hujengewa hali ya kuwa na wasiwasi na kutopenda kwenda shuleni na shule.
3. Mawasiliano: Mtoto ashirikishwe katika baadhi ya maamuzi ya ki-familia kama vile masuala ya chakula, vinywaji, maongezi n.k. Ninaposema kushirikishwa katika suala ya chakula ni katika hali ya kujenga tabia ya ushirikishwaji na kumpa uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake. Pia katika maongezi nina maana mtoto sema jambo lo lote ni muhimu kumsikiliza na siyo vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele. Tabia hiyo, itamsaidia kwa kumpatie uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.
4. Malezi: Mfumo wako wa malezi unaweza kumjenga mtoto wako au kumharibu. Kuweka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo huwajengea hali ya kujisikia kuathaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo kuwaongezea furaha na amani. Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya Imani ya kupendwa imejengwe kwenye akili zao.
Kwa hiyo, wazazi tuna jukumu kubwa sana katika kujenga watoto wetu kisaikologia katika umri wa miaka 0 hadi miaka 12. Kumjenga mtoto baada ya miaka 12 na kuendelea inakuwa vigumu sana, japo inaweza kumbadilisha.
Jiunge na blog ili upate kila makala ya blog hii.


Friday 7 October 2016

MATARAJIO YA WANANDOA KWENYE MAISHA YA NDOA

Karibuni ndugu wasomaji wa mara kwa mara wa wavuti na wale ambao ni mara ya kwanza wameingia kwenye wavuti.

Wanandoa huwa na matarajio mengi sana katika maisha yao ya ndoa hasa matarajio mazuri daima.  Maisha ya ndoa ni mchakato ambao hupita katika hatua kuu nne (4) yaani; kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Lakini si ndoa zote hupitia hatua hizo zote nne (4) baadhi hupitia hatua tatu (3) au mbili (2) kutokana na baadhi ya wanandoa kuacha kumkabidhi mlezi na mwanzilishi wa ndoa duniani yaani; Mungu. Kwenye makala hii, sitaki kuongelea sababu anuai zinazosababisha baadhi ya ndoa kutopitia hatua kuu nne (4) mzunguko wa maisha ya ndoa. Baadhi ya matarajio maisha ya iliyo katika hatua ya pili (2) ni kama yafuatavyo:-

ü  Changamoto za masuala ya kifedha.

ü  Changamoto za kimawasiliano baina yao.

ü  Changamoto zinazoletwa na wanandugu na watoto.

ü  Upweke.

ü  Kukua/kudumaa kiroho.

ü  Migogoro.

ü  Magonjwa.

Kipengere cha 4 hadi 7 nitavifafanua lakini cha 1 hadi 3 zilishavifanunua kwenye makala zangu za awali za changangamoto zinazosababishwa na wanandoa wenyewe na changamoto zinazosababishwa watu wengine wasiyowanandoa.

Upweke; Kutokana na kuongezeka kwa majukumu na uwajibikaji kwa masuala ya kifamilia maisha uliyokuwa unategemea kuwa yatakuwa daima ya amani na furaha huanza kubadilika na hapo ndipo hali ya kutaka kukaa kiupweke uanza kujitokeza ili kutafari zaidi majukumu ya kifamilia na hamu ya tendo la ndoa hupungua kwa sababu ubongo unakuwa umezingirwa na mawazo ya namna ya kutatua majukumu yaliyo mbele kama vile ada, kodi ya nyumba, gharama za usafiri kwenda na kurudi kazini, chakula nakadhalika.

Migogoro; Kutokana ndoa kuwa katika hatua ya kukua  tabia zote zilizokuwa zimevichwa na wanandoa wote uanza kudhihirika kwa sababu tabia haiwezi kufichwa daima. Tabia za kiburi, jeuri, dharau, hasira, uasherati nakadhalika uanza kuonekana na kuleta migogoro ya hapo pale katika ndoa. Hatua hii inahitaji busara na hekima kubwa hasa kwa kumshirikisha Mungu, ili kuweza kuivuka na ndoa nyingi sana huishia hatua hii.

Magonjwa; Kwa sababu za kimazingira na vyakula imekuwa ni jambo la kawaida kwa binadamu kuugua kwa muda mrefu au mfupi. Inapotokea uuguaji ni wa muda mrefu jambo ili uyumbisha sana hali ya uchumi wa wanandoa na kama hakuna upendo wa dhati basi hata misingi ya ndoa uanza kulegalega.

Mwacheni Mungu awe mtawala katika maisha yenu ya ndoa kwa maana yeye ndie muasisi ya taasisi ya ndoa hakika ndoa yenu itadumu na itakuwa kisima cha amani na furaha. Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com bure.

Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.