Kama
nilivyoeleza kwenye makala yangu ya changamoto zinazosababishwa na
wanadoa wenye mmojawapo ni mawasiliano(kutokuelewana). Hii ndio changamoto kubwa sana katika ndoa na ndio chanzo cha taraka nyingi kwa mujibu takwimu za
kimataifa. Kwa bahati mbaya tarakwimu za hapa kwetu nimeshindwa kuzipata kwa njia ya
vyanzo rasmi vya vinavyohusika na takwimu.
Kimsingi ni
kwamba migogoro inayosababishwa na kutoelewana chanzo chake kinaweza kuwa ni
mmoja wa wanadoa au wote wawili. Migogoro kikawaida ipo kwenye ndoa zote ila hutofautiana
kwa kiwango. Ipo kwenye kila ndoa kutokana na sababu za malezi na tabia za
asili za wanandoa. Na kawaida migogoro ukua kutokana na kukosa utayari wa
kuitatua kwa wanandoa wenyewe ama kwa wote wawili au mmoja wao. Inapotokea hakuna
utayari kwa wote wawili, ndoa haiwezi kudumu na kama ni kwa mmoja wao tu kuna asilimia fulani
ndoa kuweza kudumu na kama wote wako tayari kutatua ndoa hii inakuwa na
asilimia 100 kudumu.
Kama
nilivyoongea kwenye makala tajwa hapo juu. Migogoro ya kutoelewana ipo
inayotokana na mahitaji ya kawaida na ya kimwili. Leo tutaongelea migogoro inayotokana na mahitaji ya kawaida ya kimwili. Ninavyosema mahitaji ya
kawaida nina maana mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, mavazi na mahitaji mengine
ambayo siyo msingi yaani; mahitaji ya kumpendezesha mwanandoa, kushaurishwa,
kuthaminiwa n.k.
NAMNA YA KUPAMBANA NA MIGOGORO
INAYOTOKANA NA MAHITAJI YA KAWAIDA
1. Kuwa
mkweli kuhusu hali ya kipato chake.
Kuwa mkweli
wa hali yako ki-uchumi yaani; kuwa mkweli kwa mwenza wako kuhusu hali ya mapato
yako. Na ukweli huu ni vizuri ufanyike kabla ya kufunga ndoa. Ni vizuri sana
kama utauvaa uhalisia wako kipato kipindi chote cha uchumba. Hili, ni muhimu
sana kwa sababu nitakusaidia kujua kama mchumba wako ni wa kiwango chako au la.
Ukidanganya katika suala hili unakuwa umepande mgogoro ambayo itakuwa vigumu
kuusuluhisha na unakuwa umejenga hali ya kutoaminika.
2.
Onyesha kujali hitaji la mwenza wako.
Jitahidi
kujali mahitaji ya mwenza wako kwa kumtimizia hitaji lake kama uwezo unaruhusu
na kama unaona sihitaji la msingi, tafuta lugha nzuri ya kumweleza ni kwa nini
unaona hitaji lisitimizwe na bila kuonyesha dalili za kupuuza au kuonyesha
sihitaji la msingi.
3. Epuka
kuonyesha upendeleo katika kusaidia ndugu.
Katika
familia zetu za ki-afrika kuna matatizo ya kila namna kwenye familia zetu
yaani; kwa upande wa mke na mwanaume. Inapotokea kuna mahitaji upande wa
familia za upande mmojawapo ni muhimu sana kuweka uwiano wa misaada inayotolea,
ili kuepuka kuonyesha upendeleo.
4. Epuka
kuonyesha upendeleo kwa wageni wanao watembelea nyumbani.
Ni jambo la
kawaida sana ndugu wa pande zote kutamani kuwatembelea wanandoa katika hali ya
amani au matatizo. Ni vizuri kujitahidi kutoonyesha unyanyapaa kwa wanandugu wa
upande mmoja hali hii inaweza kuleta mgogoro mkuu.
5. Epuka
kuonyesha dharau dhidi ya mila na desturi za mwenza wako.
Inapotokea
wanandoa ni makabila tofauti ina maana watakuwa wamekulia kataika mila na
desturi tofauti. Mila na desturi uhusisha namna ya kuongea, mapishi, tofauti za
ki-maendeleo baina ya kabila moja na nyingine. Si vizuri kuonyesha dharau hata
kama ni katika hali ya utani kwa sababu hiyo huonyesha hisia zako dhidi ya
mwenzako hata kama utasema unamtania.
6. Epuka
utani unaoeleka kweli uhalisia kimaumbile.
Jitahidi
kuepuka utani unaohusiana na maumbile kama vile watu wafupi au wanene wana
kasoro 1,2,3 n.k. wakati ukijua kwamba mwenza wako nao ana maumbile kama hayo.
Utani kama huo hufanya mtaniwa kujisikia vibaya na kuleta migogoro katika ndoa.
7. Kushaurishwa
katika mambo ya msingi ki-familia.
Kitabia kila binadamu anapenda
kuthaminiwa katika mambo tofauti tofauti kama kazi zake, ushauri n.k. Katika mambo ya msingi ya maendeleo ya kifamilia kama vile
ununuzi wa kitu cho chote cha kifamilia kama vile samani, na vitu vingine
muhimu katika maisha yetu ya kila siku.
Ili kuendelea kupata makala hizi weka jina lako na barua pepe kwenye kisanduku kidogo mkono wa kulia.
Ili kuendelea kupata makala hizi weka jina lako na barua pepe kwenye kisanduku kidogo mkono wa kulia.