Friday 11 September 2015

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA mwendelezo

Samahani sana sana wasomaji wangu wa blog hii kwa kutokutoa makala kila juma kama inavyopaswa. Hii inatokana na sababu mbalimbali za kimaisha za hapa na pale. Naomba mnisamehe kwa kutoonekana kwa kipindi kirefu bila kuwataarifa. Leo naendelea na mada niliyoicha huko nyuma.
3. Kumtafuta mchumba kumtarajiwa
Ili kumpata mchumba mzuri miongoni mwa marafiki zako wa kike/kiume ni vizuri kutokuonyesha mapema kwamba dhamira yako ya kumtafuta urafiki dada/kaka huyu ni kwa nia ya kumtafuta uchumba. Hili ni muhimu, ili asiweze kuficha baadhi ya tabia zake zisizofaa kuwa mchumba na hatimaye kuwa mke/mme.  Tabia hizo ni kama vile dharau/lugha chafu kwa wazazi ,kwa ndugu, marafiki, mchumba, uchafu n.k. kutokuwa mchaa Mungu wa dhati, uwongo, mchonganishaji,umbeya,  umalaya, kuthamini mali kwa kupitiza kiasi cha kukosa utu, nakadhalika.
Ukipata mchumba mwenye sifa tajwa hapo juu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu utakuwa umepata mchumba bora wa kuweza kuwa mke. Pamoja na sifa zote hizo mchumba mzuri/bora ni yule unayejisikia raha na fahari kuwa nae hata kumtambulisha kwa ndugu na marafiki.  Yaani, awe nakidhi matamanio yako ya mchumba  wa ndoto yako.
Nakaribisha maoni yenu ndugu wasomaji wa blog hii.