Monday 21 July 2014

NYENZO ZA KUSTAWISHA NDOA

Napenda kuchukua nafasi hii, kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi hii adimu ya kuwaandikieni makala hii fupi. Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji  wangu wapendwa wa mabara yote kwa kuendelea kunitia moyo kwa ushauri na maoni yenu mazuri,  nawaombeni muwaalike na marafiki zenu kusoma makala za blogu hii.
Kwa tafsiri isiyo rasmi nyenzo ni kifaa cha kufanyia kazi. Kwa musktadha wa makala hii nyenzo imetumika kwa maana ya kanuni. Napenda kutajwa nyenzo za kustawisha ndoa kwamba ni kama zifuatavyo: -

a)    Kubali kuwa wewe ndio chanzo cha mgogoro
b)    Kutokata tamaa (tumaini)
c)     Kusamahe
d)    Beba hisia za mwenzako (Empathy)
e)     Kujitoa
Ufafanuzi wa nyenzo hizo ni kama ifuatavyo: -
Kubali kuwa wewe ndio chanzo cha mgogoro; Ni kawaida ya wanandoa kusukumia lawama kwa ndugu, jamaa, marafiki  na watoto kuwa ndio chanzo cha migogoro katika ndoa. Jambo ili si sahihi kwa sababu ndugu, jamaa, marafiki na watoto ni matokeo ya ni nyi kuwa mwili mmoja yaani; kufunga ndoa. Migogoro yo yote inayojitokeza katika ndoa chanzo chake ni wanandoa wenyewe; ndugu, jamaa, marafiki na watoto wao ni wachocheze tu ili kukoleza moto ili uweka zaidi. Hapa nina maana kwamba chanzo cha kutoa siri au kasoro zo zote zilizomo ndani ya ndoa ni wanandoa wenyewe. Kwa hiyo, wanandoa kama watakuwa radhi kuongelea na kuzitafutia suluhu changamoto zao za kwenye ndoa kisirisiri wanakuwa na asilimia mia moja ya kustawisha ndoa yao bila shaka yo yote.
Kutokata tamaa; Maisha yamejaa changamoto nyingi sana na changamoto hizi zipo kwa ajili ya kukufanya uweze kufikia mafanikio yaani; ni daraja kuelekea kwenye mafanikio. Changamoto katika ndoa zipo nyingi sana na nyingi huletwa na wasiliano mabovu baina ya wanandoa wenyewe (Kwa uelewa zaidi juu ya hili bofya hapa), hali ya uchumi, ndugu, jamaa, marafiki nakadhalika. Jambo kubwa hapa ni kuwa na matumaini ya suluhu na kuitafuta dhidi ya changamoto zo zote zinazojitokeza kwa sababu hakuna changamoto isiyo kuwa na njia ya utatuzi.
Kuwa tayari kusamehe; Kusamehe ni agizo la Mungu na pia ni ishara ya busara. Mme/mke si malaika kwa hiyo yeye kufanya makosa ni jambo la kawaida la kibinadamu. Jitahidi kusamahe kadri uwezevyo na muelimishe mwenzako kadri uwezevyo mpaka ufike mahali pa kumuelewa vema. Ili zoezi mnatakiwa mlifanye maisha yenu yote ya ndoa kwa sababu makosa mengi hufanywa pasipo kukusudia.
Beba hisia za mwenzako (Empathy); Jitahidi kumuelewa mwenzako na beba hisia zake. Kwa kufanya hivyo, itakuwa rahisi sana kudumisha ndoa yenu kwa maana haitakuwa rahisi kumfanyia ukatili au kumlazimisha kufanya jambo ambalo wewe mwenyewe usingependa kufanyiwa. Yaani hisia za upendo na huruma zitatawala maisha yenu daima.
Kujitoa; Changamoto za ndoa ni nyingi sana na ili ndoa iweze kudumu inahitaji wanandoa wote kwa pamoja wawe na moyo wa kutojitoa kwa lengo la kuhakikisha kwamba ndoa yao inadumu, bila hivyo ndoa nyingi zisingekuwa zinadumu. Ninaposema kutojitoa nina maana kuwa radhi kukubaliana na mambo hata yasiyokupendeza ili mradi tu ndoa yao iwe endelevu. Vipengere vyote hapo juu (a mpaka d) vinawezekana tu iwapo kutakuwa na moyo wa kujitoa.
Mweke Mungu mbele katika maisha yenu ya ndoa kwa maana yeye ndie muasisi ya taasisi ya ndoa hakika ndoa yenu itadumu na itakuwa kisima cha amani na furaha. Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala zenye maarifa tele ya masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.


No comments:

Post a Comment