Friday 29 April 2016

MAMBO SITA (6) YANAYOWATIA HOFU WANAWAKE KATIKA NDOA


Karibu ndugu wasomaji wa wavuti hii, leo napenda kuongelea mambo sita yanayowatia hofu wanawake kwa waume zao pamoja ustawi wa ndoa zao. Kutokana na tafiti mbalimbali na uzoefu wa kimazingira kuna hofu nyingi wanazokuwa nazo wanawake dhidi ya waume zao hasa kwa ndoa changa na ambazo hazikupitia hatua ya uchumba wa muda mrefu. Kama iliyohada mke na mme hukutana wakiwa wote ni watu wazima waliyokulia katika mazingira, utamaduni na familia tofauti wakapendana na kufikia maamuzi ya hiari ya kufunga ndoa. Kutokana na mzingira, makuzi, utamaduni, mtazamo n.k. watu wanapokuwa wameamua kufunga ndoa hutokea hofu za kimahusiano za hapa na pale ambazo kila mmoja hujitahidi kuziondoa. Tafiti za kisaikolojia zinasema hujengwa katika mtazamo hasi. Baadhi ya hofu hizo ni kama zifuatazo: -

©       Hofu ya kutoridhishwa katika tendo la ndoa.

©       Hofu ya kutomridhisha mmewe katika tendo la ndoa.

©       Hofu ya mmewe kupotea hamu ya ndoa.

©       Hofu ya mmewe kumkinai na kuanza michepuko.

©       Hofu ya mmewe kutobadilika katika baadhi ya matendo yasiyompendeza.

©       Hofu ya kutokua kiroho kama wanandoa.

Naomba nifafanue kidogo juu ya hofu hizo sita hapo juu.

©       Hofu ya kutoridhishwa katika tendo la ndoa na mmewe.

Kutokana tafiti na ushahidi wa kimazingira ndoa nyingi zinazofungwa sasa zinakutanisha wanandoa wenye uzoefu wa viwango tofauti wa tendo la ndoa ambao wameupata kwa wanaume wengine tofauti na mme anayefunga nae ndoa. Hii inatokana na jamii kukosa maadili ya ki-utamaduni na kidini upande wa malezi.

Wanawake wengi wanaingia katika ndoa kwa kufuata hali ya uchumi ya muoaji au kutokana na umri kuwatupa mkono na hivyo kujiingiza katika ndoa na shinikizo hizo mbili, kwa sababu wenye kukidhi haja za tendo la ndoa hawahitaji kuwaoa au ni waume wa watu. Kutokana na uzoefu wa kukutana na wanaume mbalimbali na wengi kutokidhi haja zao za tendo la ndoa huingia katika ndoa na hofu hii. Tafiti zinaonyesha kwamba mwanamke akitembea na wanaume kumi ni mmoja au sifuri wenye uwezo wakumridhisha katika tendo la ndoa. Na hii ndio inayowafanya kuingia katika ndoa na hofu hiyo, licha ya kwamba asilimia kubwa ya ndoa za siku hizi wanandoa wengi huingia kwenye ndoa wakiwa wanajuana vizuri. Lakini huingia kwenye ndoa kwa  kutegemea kwamba wenza wao watabadilika na kuweza kuwaridhisha kadri watakavyoendelea kuishi.

©       Hofu ya kutomridhisha mmewe katika tendo la ndoa.

Kama nilivyongea kwenye kipengele cha hapo juu ya uzoefu wa kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Pamoja na uzoefu wa kuachwa na wanaume mbalimbali zikiambatana na kashfa mbalimbali kutoka kwa wanaume waliyowaacha huwajengea hofu ya kukidhi haja ya waume zao ya tendo la ndoa. Na kwa wanandoa ambao hawaongelei kabisa juu ya tendo hilo na hawana maandalizi kabla na tendo la ndoa huishi katika hofu hiyo maisha yao yote.

Hii ni changamoto kubwa sana katika ndoa nyingi dunia nzima, ndio talaka zinazidi kuongezeka.

©       Hofu ya mmewe kupoteza nidhamu ya ndoa.

Kawaida ukiwa katika ndoa kuna nidhamu ambayo lazima izikatiwe kama vile muda wa kurudi nyumbani, matumizi, ulaji nakadhalika kwa ndoa ambazo wanandoa wanaheshimiana. Katika ndoa ambayo wanandoa wanheshimiana kila mmoja ni mlinzi wa mwenzie yaani kuagana na kujulishana kila mmoja alipo inakuwa ni jambo la kawaida kabisa.

Kutokana na ndoa nyingi kupoteza nidhamu mme kulala nje, kuchelewa kurudi nyumbani n.k. wanawake wengi huwa na hofu ya ndoa zao kuingia katika misukosuko ya aina hii.

©       Hofu ya mmewe kumkinai na kuanza michepuko.

Kutokana na hofu ya kutokumridhisha mmewe hofu ya kukinaiwa na mmewe hujitokeza.

©       Hofu ya mmewe kutobadilika katika baadhi ya matendo yasiyompendeza.

Kutokana na sababu ya kuingia kwenye ndoa kutokana shinikizo nilizozitaja hapo juu, wanandoa wengi hugundua kwamba wenzio wao mara nyingine wanatabia ambazo ni kero kama vile ubishi, uchelewaji kurudi nyumbani bila taarifa, kufanya mambo ya msingi bila kumshirikisha mwenza, kutopenda kula nyumbani n.k. Mambo haya kimsingi huleta msongo wa mawazo pale ambapo mme anaambia kujirekebisha lakini anakuwa mgumu kubadilika kwa sababu ya tabia za mfumo dume.

©       Hofu ya kutokua kiroho kama wanandoa.

Katika nchi hasa za ki-afrika kuna ndoa za aina tatu(3):

 ü  Kidini

ü  Kiserikali

ü  Kimila

Tafiti zinaonyesha kwamba ndoa nyingi zinafungwa kidini, kutokana na hofu nilizozitaja hapo juu suluhisho pekee linategemea imani ya wahusika. Hili kutatua matatizo hayo hapo hali ya imani ya kidini ya wanandoa ni muhimu sana kwa maana taasisi hii mwanzilishi ni Mungu mwenyewe kwa mujibu vitabu vya kidini. Kwa hiyo, Imani inapokuwa chini ni vigumu sana kutatua hofu zinazojitokeza katika taasisi hii muhimu sana.

Nimeongea kifupi kwenye kila kipengele na ninaamini kila jambo linasuluhisho katika dunia hii. Naomba nipate maoni yenu.

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment