Monday, 25 April 2016

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA mwendelezoHabari za siku nyingi ndugu zangu wasomaji wa wavuti hii. Samahani sana kwa ukimya wa muda mrefu sana, kwa sababu ni siku nyingi sana nimeanza makala hii, naomba leo niimalize kwa kuiongelea kwa kifupi ili tuendelea na makala zingine. Michakato inayofuatia ni kama ifuatavyo: -

4.      Kumshukuru Mungu

Ki-imani tunaamini kwamba mke/mme mtu hupewa na Mungu hasa kama umemshirikisha/ulimuomba kama mchakato unavyoeleza hapo juu. Na hii, ni kwamba kuoa/kuolewa ni mpango wa Mungu wa kuongeza kizazi cha wanadamu.

5.      Msichana/Mwanamke kuwajulisha wazazi wake 

Baada ya kumshukuru Mungu na kuafikiana kwenda kuwajulisha wazazi juu ya azma ya kuwa mke na mme hatua inayofuta ni msichana/mwanaume kwenda kuwajulisha wazazi juu ya suala la kumpata mwenza.

6.      Mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi wa mwanamke kuchumbia

Hatua ya mwisho ni wazazi wa mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi wa msichana/mwanaume kwenda kuchumbia ili hatimaye waweze kufunga ndoa.

Naomba nipate maoni yenu kuhusu makala husika.

 
 

No comments:

Post a Comment