Monday, 9 June 2014

MANENO/TABIA 7 HATARISHI KWA HUSTAWI WA MAHUSIANO

Ndugu msomaji leo napenda niongelee maneno/tabia ambayo ni hatarishi kwa wanamahusiano (wanandoa au wachumba). Maneno hayo kwenye mabano nilishayatatolea tafsiri isiyo rasmi kwenye makala yangu ya utambulisho wa blogu. Kabla sijaenda mbali naomba leo niwape tafsiri ya ndoa kwa mujibu wa mtaalamu  wa mambo ya ndoa Ndugu Nancy Van Pelt katika kitabu chake kiitwacho “To have and to hold” “A guide to successful marriage”. Katika kitabu hiki ndoa imetafsiriwa kwamba ni  muunganiko wa upendo wa mwanamke na mwanaume katika nyanja zote za maisha na kwamba munganiko huu ni wa kimwili, kihisia, kiakili na kiroho na kwamba taasisi hii ni ya siku nyingi sawa na uwepo wa binadamu katika sayari hii.
Katika mahusiano kuna baadhi ya maneno hayafai kumwambia mwenza kwa sababu mara nyingi yameokana kuvuruga mahusiano mengi sana. Baadhi ya tabia/maneno hatarishi ni kama zifuatavyo:-
1.       Kumwambie mwanza wako wewe hujui Kitu; Neno ili kwa ujumla halifai kulitumia kumwambia mwenza wako kwa sababu tafsiri yake ni pana sana na huibua hisia nyingi sana kwa aliyeambiwa. Mara nyingi mwambiwa hujisikia kwamba hajui mambo ya unyumba. Kwa hiyo, kumuondolea unyonge ni busara ukatoa ufafanuzi ni mambo gani unaona mwenza wako hajui, na unafanyaje kumrekebisha kama mwenza wako.
2.       Kumsifia mwanamke/mwanaume mwingine; Jitahidi sana kuepuka tabia ya kumsifia mwanamke/mwanaume yo yote kimapana, hii itakuletea matatizo makubwa katika mahusiano yenu kwa sababu wa wivu ambao mara nyingi utawala mahusiano.
3.       Maneno yakudhihaki maisha ya nyumbani kwa mwenza; Maneno ya kudharau familia ya mwenza wako ki-uchumi, ki-utamaduni, ki-desturi nakadhalika.
4.       Utani dhidi ya mwenza unaogusia maumbile yake halisi; Ninaposema maumbile ninamaanisha ufupi, unene, wembamba, nakadhalika. Utani wo wote wenye kuonyesha dhihaka dhidi ya tabia zinazoenda na maumbile haya zinaweza kuleta matatizo makubwa kwenye mahusiano. Maneno kama watu wafupi Bwana, watu wanene Bwana nakadhalika. Kwa sababu suala la maumbile halina uchaguzi Mungu ndie anayepanga.
5.       Lawana za mara kwa mara dhidi ya mwenza wako; Kwa asili kila binadamu hupenda kusifiwa pale anapofanya jambo zuri na kusahihishwa si kulaumiwa pale anapokosewa. Si vizuri kulaumu mwenza wako anapokuwa amefanya jambo/kitu ambacho kwako wewe mpokeaji hakijakufuraha. Tafuta lugha nzuri ya kumweleza mwenza wako pale anapokuwa amekosea ki-mapishi, zawadi, manunuzi yo yote ya kifamilia, usafi wa nyumba, nakadhalika, tabia kama hiyo ukatisha tamaa.
6.       Kutoa siri za ndani nje; Ndoa ni mchakato na kuna mambo mengi ambayo wanandoa wanatakiwa kuelimishana ili ndoa iweze kuendeleakustawi na kudumu. Katika mambo ambayo wanandoa hawapaswi kutoa nje ni pamoja na mambo yanahusu unyumba. Ni jambo la hatari sana kwa mwanandoa kutoa siri za masuala ya unyumba kwa sababu tabia hii mara nyingi huishia kubomoa nyumba. Siri hii, haifai kutolewa nje iwe ni kumsifia au kumlaumu mwenza kuhusiana na suala la unyumba sio vizuri kwa mstakabali wa ndoa.
7.       Kuzaa nje ya ndoa; Ni dhairi kwamba wanandoa wengi wanatoka nje ya ndoa kinyume na agano la ndoa na pia maagizo ya Mungu takwimu zinaonyesha 55% ya wanandoa wanatoka nje. Taarifa hii, ni kwa mujibu wa takwimu mbalimbali za tafiti katika nchi mbalimbali duniani. Pamoja na ukweli kitendo cha mwanandoa kuzaa nje ya ndoa akiwa ndani ya ndoa ni jambo ambalo linaweza kuvunja ndoa bila kujali ni nani kafanya hivyo yaani; mme au mke.

Ili kupata maarifa ya kukabiliana na changamoto za mahusiano na kupata maarifa ya kustawisha na kudumisha mahusiano yako jiunge na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kwa kupitia kwenye airtel 0784190882 au Tigo pesa 0719841988.

Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA.


No comments:

Post a Comment