Monday 2 June 2014

DALILI ZA MAHUSIANO YANAYOENDA MRAMA

Napenda kuchukua nafasi hii, kuwashukuru wale wote walitoa maoni na ushauri mbalimbali kuhusiana na makala zilizotangulia.
Jambo lo lote kabla halijatokea kunakuwa na dalili au ishara fulani za kuonyesha kutokea suala fulani. Kwa mfano kuna msemo uliyozooleka wa kwamba dalili za mvua ni mawingu ipo na misemo mingine inayofanana kama hiyo katika jamii. Katika suala la mahusiano hasa yaliyofikia hatua ya ndoa kuna dalili huwa zinajitokeza kuonyesha kwamba hali si shwari au inaelekea mwisho. Katika hali ya kawaida ya maisha yo yote kunakuwa na mzunguko huu; kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Pia katika mahusiano kuna yanayopita hatua zote hizo nne (4) na nyingine hupitia hatua tatu (3) au mbili (2) tu.
Leo naongelea mahusiano ambayo yamefikia hatua ya pili (2) yaani; kukua. Dalili za kuonyesha kwamba mahusiano yanaenda mrama kwa mujibu wa tafiti mbalimbali  ni kama zifuatazo: -
1.       Ugomvi wa mara kwa mara wa bila sababu ya msingi; Ugomvi wa mara kwa mara unaotokana na sababu zisizo za msingi ni dalili ya mahusiano yanayo kwenda mrama. Ugomvi unaweza ukasababishwa na chakula, watoto, nguo nakadhalika. Na mara nyingi sababu zinakuwa siyo hiyo inayoongelewa,  bali ni kutokana na maalimbikizo ya makosa fulani madogo ya hapo nyuma au mmoja wa wanamahusiano amepata mtu anayempotosha/kumdanganya.
2.       Dharau za kupitiza na kejeli za hapa na pale; Maneno ya dharau mpaka matusi huanza kujitokeza kwa wanahusiano ki waziwazi, ilimradi tu kuonyesha kwamba uhusiano una kwenda mrama. Maneno kama vile wewe si cho chote, ningekujua ni singeolewa na wewe, kulala nje,kuondoka nyumbani bila taarifa, kurudi usiku wa manane bila taarifa yo yote kwa mwenza, kutukana ndugu wa upande wa mwenza, kunyimwa unyumba, niko hapa kwa ajili ya watoto tu  n.k.
3.       Kuomba kuungwa mkono na watoto/wanandugu kwenye ugomvi; Tabia ya wanahusiano kuingiza watoto/wandugu kwenye ugomvi kwa kusema mwenza ndie chanzo cha ugomvi. Hii inaambatana na kutoa siri za ndani za mwenza kwa watoto/wanandugu n.k.
4.       Kuhama chumba; Kutokana na uhasama kuwa mkubwa kuamiana kuondoka kwa visngizo mbalimbali wanamahusiano hufikia hatua ya kulala vyumba tofauti. Hutokea  mwanzilishi wa ugomvi uamua kuhamia sebuleni kama vyumba ni vichache au chumba cha watoto.
5.       Madai ya kuachana ;Baada ya hatua hizo hapo juu hatua inayofuata ni ya kudai kuachana au kwenda kanisani/msikitini kueleza matatizo yao ya mahusiano. Suluhu za wachungaji na masheikh  mahusiano yanapofikia hatua hii, mara nyingi hazizai matunda. Mwanzilishi wa ugomvi uamua kwenda mahakamani kudai taraka upande serikali.
Mahusiano yanapofikia hatua ya tano (5) kama mmefunga ndoa ni vizuri kutafuta kiini cha matatizo hayo na kupiga magoti na kuomba Mungu aingilia kati kwa kuondoa ibilisi kati yenu. Pia kwa kusoma  makala za ushauri wa migogoro ya mahusiano kwenye blogu ya http://mkombozi-mahusiano unaweza kupata suluhisho kwa kuwa mwanachama.  Ada ya uanachama wa blogu tajwa hapo juu ni TZS. 10,000.00 na unailipia kwenye TiGO pesa ya 0719841988 au airtel money 0784190882 baada ya kulipa tuma e-mail address yako ya google kwenye namba yo yote kati ya hizo. Kama huna e-mail address ya google tunakushauri ufungue e-mail address husika.
 Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


No comments:

Post a Comment