Friday 20 June 2014

UNAPOINGIA KWENYE NDOA JIANDAE PIA NA YATOKANAYO NA NDOA

Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kumshukuru mwenye Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii adimu ya kuwaandikieni makala hii fupi. Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji  wangu wapendwa kwa kuendelea kunitia moyo kwa ushauri na maoni yenu mazuri, naomba muendelee na moyo nawaombeni muwaalike na marafiki zenu kusoma makala za blogu hii.
Leo hii napenda kuongelea sababu za ndoa nyingi kuwa na migogoro inayoishia kuachana. Tafiti nyingi sana zinaonyesha kwamba wastani wa  ndoa 65% zina migogoro mingi ambayo inaweza kuepukika kwa kupata ushauri muafaka. Takwimu hiyo ni kwa mujibu wa tarakwimu kwenye nchi zilizoendea na zinazoendelea. Baadhi ya sababu za ndoa nyingi kuingia katika matatizo ni kama zifuatazo: -

1.    Wanandoa wengi wanaingia kwenye ndoa na mtazamo wa kwamba ndoa ni raha tupu; Wanaume/wasichana wengi wamekuwa wakiingia kwenye ndoa na mtazamo wa kwamba maisha ya ndoa ni raha tupu kama inavyokuwa wakati wa uchumba. Yaani tabia za kiuchumba kama vile kwenda kula Hoteli, kutoka (outing), kutumia takeaway nakadhalika badala ya kupika. Kwa sababu ya huo mtazamo finyu,  wanandoa wengi  wanakuwa hawajajiandaa kisaikologia kukabiliana na migogoro. Kwa hiyo, migogoro midogo midogo kama vile kuambiwa hakuna hela ya kufanya starehe ndogo ndogo za kimazoea ya kiuchumba zinapoanza kujitokeza katika ndoa, mmoja wa wanandoa  huishia kuchanganyikiwa na kuhisi kusalitiwa na wenzi wao. Kutokana na hisia hizo hasi  mawazo ya kujiamini  dhidi ya hisia hizo husababisha nyumba kuanza kuyumba. Kwa sababu ya hisia  hizo hasi mawasiliano ya kawaida kama wanandoa huingia kasoro.
2.    Wanandoa wengi huingia kwenye ndoa kwa tamaa ya mali; Ni ukweli uliyo wazi kwamba kuna wanaume/wasichana wengi huingia katika mahusiano na hatimaye ndoa kwa tamaa tu ya mali za mmoja wa mwanandoa. Ndoa kama hii, mhimili wake unakuwa ni mali za mmoja wa wanandoa kwa hiyo, inapotokea kwamba hizo mali zimeisha ndoa huanza kuteteleka au kuanguka.
3.    Tendo la ndoa; Wanandoa wengi huingia kwenye ndoa wakiwa na imani kwamba watafanya tendo la ndoa kila siku na mara kadhaa kwa siku.  Inapotokea mmoja wa wanandoa hapendi utaratibu wa kufanya tendo la ndoa kwa utaratibu huo,basi  hili nalo huwa chanzo cha kuitilafiana. Iwapo wanandoa wana  mtazamo unaofafana basi hilo haliwi tatizo na mmojawapo akiwa kinyume chake inakuwa  ni chanzo cha mgogoro. Hili ni mojawapo wa sababu kubwa inayoleta matatizo katika ndoa nyingi. Kimsingi ni kwamba binadamu tunatofautiana  sana katika uhitaji wa tendo la ndoa. Kwenye suala hili ni vizuri kufahamiana vema kimwili, ili kudumisha mstakabali ya ndoa. Hoja ya tendo la ndoa ni changamoto kubwa sana katika ndoa hasa kama wanandoa si wa wazi. Yaani hawako tayari kuongelea masuala yanayohusiana na tendo la ndoa kiuwazi.
4.    Kutokuwa na imani ya dini; Ni ukweli usiyojificha  kwamba imani zote za kidini zinatufundisha kuvumiliana na kusameheana na kumkubali kila binadamu kwa namna alivyo na huu ndio msingi mkuu wa imani zote.Yaani mpende kila binadamu kwa namna alivyo.  Kwa maana hiyo, wanandoa wanaoishi pasipo na kumshirikisha Mungu ni rahisi sana kuingia katika migogoro kutokana na migogoro isiyo na msingi.
5.    Kuigiza tabia na uchumi; Baadhi ya wanandoa huigiza tabia na hali za kiuchumi tofauti na uhalisia wao, ili tu, waweze kuwapata watu wanao watamani kuwa wenzi wao.  Ninaposema kuigiza tabia nina maana kujifanya mpole, mchaa Mungu, mkarimu nakadhalika wakati kiuhalisia hauko hivyo. Ninaposema kuigiza kiuchumi nina maana kujifanya una uwezo wa kiuchumi na yaani; pesa kwako siyo tatizo una miradi, majumba, magari nakadhalika wakati huna kitu. Tabia hii ya kuigiza ni haifai kwa sababu mwenza wako anapogundua kwamba ulikuwa una mdanganya ndoa itakuwa imeingia hitilafu kubwa.
Mambo yote hayo niliyoyataja hapo juu yanaweza kuepukwa,  iwapo utakuwa mtafiti  na utamshirikisha Mungu katika mipango yako ya kuingia kwenye ndoa.  Na pia nakushauri kujiunga na blogu  ya  http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com  kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Aairtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala za ushauri makini wa masuala ya mahusiano.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


No comments:

Post a Comment