Tuesday, 12 August 2014

LENGO LA NDOA

Habari za majukumu mbalimbali ya kiuchumi ndugu wasomaji wa blogu hii, bila shaka nyote ni wazima kwa uweza wa mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa wale ambao afya zao zimetetereka kidogo Mungu yu pamoja nanyi mtapona.
Leo napenda kuongelea malengo la ndoa kwa muktadha wa Mungu ambaye ndie muasisi wa ndoa katika bustani ya Eden. Kwa lengo makala hii, ndoa ninayoiongelea hapa ni ya watu wa jinsi tofauti yaani; mwanamke na mwanaume. Sababu za msingi za kuweka ndoa ni kama zifuatazo: -
Ø  Kuondoa upweke.
Ø  Kusaidiana kupambana na changamoto za kimaisha.
Ø  Kujenga familia.
Ø  Kuendeleza kizazi.
Ø  Kukidhi tamaa ya mwili.
Ø  Kuakisi upendo wa Mungu.
Sababu hizo sita (6) ninaweza kuzifafanua ifuatavyo: -
Kuondoka upweke; Kama nilivyoongea kwenye utangulizi Mungu ndie mwanzilishi wa taasisi hii ya ndoa katika Bustani ya Eden. Binadamu wa kwanza kuumbwa Dunia alikuwa ni Adam baada ya kuona yu mpweke Mungu alimuumba Hawa kuwa msaidizi wake kutoka kwenye ubavu wa Adam.
Kusaidiana kupambana na changamoto za kimaisha;Maisha yanachangamoto nyingi sana za kiuchumi, kiafya, ki-imani nakadhalika ukipata mke au mme ambae ni chaguo sahihi/bora atakusaidia kupambana na changamoto za kimaisha. Mke na mme sahihi hupatikana kwa msaada wa mwenyezi Mungu. Kwenye makala ya namna ya kupata mchumba kuna maelezo ya kujitosheleza kuhusu mada hii. Makala hii, inapatikana kwenye blogu yangu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ambayo utaratibu wake wakujiunga nitawafahamisha hapo mbele.
Kujenga familia; Familia ni baba, mama na mtoto/watoto. Ni dhahiri kwamba mke na mme kwa majaliwa ya mwenyezi Mungu wakifahamiana kimwili matokeo yake ni mimba hatimaye mtoto au watoto kutegemea na watakavyokuwa wanaamua wao wenyewe. Kwa hiyo kujenga familia ni mmojawapo wa lengo la kufunga ndoa japo kwa baadhi ya watu mtoto au watoto si lengo lao!
Kuendeleza kizazi; Kusudi la mwenyezi Mungu kuweka mbegu kwa viumbe vyote hai wakiwemo na binadamu ni ili kuendeleza kizazi cha uumbaji wake. Kila kiumbe kiliumbwa na mbegu ya kukiendeleza yaani; mmea, wanyama pamoja na binadamu, ndege wa angani, viumbe wa majini nakadhalika.
Kukidhi tamaa ya mwili;Binadamu aliyepevuka ameumbwa na tamaa ya kufanya tendo la ndoa. Ndoa imeweka na mwenyezi Mungu kuwa ni unganiko halali la kukidhi tamaa ya mwili ya tendo la ndoa kwa wanandoa.
Kuakisi upendo wa Mungu; Mungu ni pendo na hii ndio sifa kuu ya Mungu ambayo anapendo wanadamu wawe nayo. Ndoa uunganisha mme na mke kuwa mwili mmoja kimwili, kihisia, ki-imani vyote hivi vikiwa vimejengwa katika msingi wa upendo. Mme na mke wataachana na wazazi wao na kuungana kuwa mwili mmoja kwa sababu ya kupendana.
Mkabidhini Mungu awe kiongozi wa maisha ya ndoa yenu siku zote kwa maana yeye ndie muasisi ya taasisi ya ndoa,  hakika ndoa yenu itadumu na itakuwa kisima cha amani na furaha na kielelezo cha mfano kwa ndoa nyingine. Na pia nakushauri ujiunga na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com kwa TZS. 10,000.00 kupitia huduma ya Tigo na  Airtel Money  kupitia  0719841988 na 0784190882 upate makala zenye maarifa tele ya masuala ya mahusiano na ushauri.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA IMARA. Pia nakaribisha maoni yako kuhusu makala za blogu hii.

No comments:

Post a Comment