Habari za siku
nyingi ndugu zangu wasomaji wa wavuti hii. Samahani sana kwa ukimya wa muda
mrefu sana, kwa sababu ni siku nyingi sana nimeanza makala hii, naomba leo
niimalize kwa kuiongelea kwa kifupi ili tuendelea na makala zingine. Michakato
inayofuatia ni kama ifuatavyo: -
4. Kumshukuru Mungu
Ki-imani
tunaamini kwamba mke/mme mtu hupewa na Mungu hasa kama umemshirikisha/ulimuomba
kama mchakato unavyoeleza hapo juu. Na hii, ni kwamba kuoa/kuolewa ni mpango wa
Mungu wa kuongeza kizazi cha wanadamu.
5. Msichana/Mwanamke kuwajulisha wazazi
wake
Baada
ya kumshukuru Mungu na kuafikiana kwenda kuwajulisha wazazi juu ya azma ya kuwa
mke na mme hatua inayofuta ni msichana/mwanaume kwenda kuwajulisha wazazi juu
ya suala la kumpata mwenza.
6. Mvulana/mwanaume kwenda kwa wazazi
wa mwanamke kuchumbia
Hatua ya mwisho ni wazazi wa mvulana/mwanaume kwenda
kwa wazazi wa msichana/mwanaume kwenda kuchumbia ili hatimaye waweze kufunga
ndoa.
Naomba
nipate maoni yenu kuhusu makala husika.
No comments:
Post a Comment