Wednesday, 29 April 2015

MCHAKATO WA KUPATA MCHUMBA- mwendelezo

1.       Kumuomba Mungu Akupatie Mchumba.
Ukweli usiyopingika kwamba watu wengi wanajua kuombea chakula au kuomba Mungu pale wanapoona kuna dalili ya hatari mbele. Maombi ya chakula huwa ni ya juu juu tu kwa sababu ni ya mazoea lakini maombi ya kumuomba Mungu pale unapohisi/kuona hatari huwa ni yahisia sana na yenye unyenyekevu na kujitoa ndani yake.
Katika maombi ya kumuomba Mungu kukupatia mke hayapaswi kuwa ya juu juu hata kidogo bali yanapaswa kuwa maombi ya kujitoa sana kwa sababu maisha ya binadamu yo yote yanaweza kujengwa au kuharibika kutegemea kapata mke au mme mwenye kufanana nae kinahisi na matarajio au la. Mali na vitu vingine vyote mtu hupewa na wazazi wake bali mke mwema hupewa na Mungu. Sentensi hiyo ya mwisho ni kwa mujibu wa maandiko mmojawapo wa vitabu vya Mungu.
Maombi ya kuomba mke kwa Mungu yanapaswa kuwa ya kujitoa yenye kuonyesha unyenyekevu mkubwa na kufunga na ikiwezekana kuwashirikisha na watu ambao mna Imani moja. Katika maombi unashauriwa kuainisha sifa unazotaka awe nazo mchumba wako zenye kurithisha matamainio yako.
2.       Kutafuta rafiki ambaye anaweza kuwa mchumba mtarajiwa.
Kikawaida kwa mujibu wa maandiko ya vitabu vitakatifu atafutae uona na ombae hupewa.  Ukiisha kumuomba Mungu atakupatia macho ya kuona kile ulichokiomba yaani; msichana/mwanamke au mvulana/mwanaume wakukufaa kuwa mchumba na hatimaye kuwa mke/mme. Kwa urahisi wa kufanya uchaguzi wa mchumba anayefaa au unayefanana naye ni vizuri ukawa na ukaribu/urafiki na wavulana/mwanaume au wasichana/wanawake wengi. Urafiki huu ni vizuri ukawa ni urafiki wa kaka na dada pasipo makubaliano yo yote yakutaka kuwa wachumba miongoni mwa marafiki hao bila shaka yo yote Mungu atakuonyesha ni yupi unayefanana nae na wakukufaa kuwa mchumba wako.
Ili kupata uchaguzi bora wa kitu cho chote ni lazima uwe na wigo wa kufanananisha kati ya hiki na kile kipi ni hivyo hivyo pia katika masuala ya uchumba.
Makala ijayo tutaendelea na ufafanuzi wa vipengere vingine

No comments:

Post a Comment