Sunday 11 May 2014

UTAMBULISHO WA BLOGU

Kabla sijaeleza madhumuni ya blogu hii ningependa kutoka tafsiri  isiyo rasmi ya maneno makuu katika jina la Blogu hii yaani; Ushauri, Changamoto, Ndoa na Uchumba.

Ushauri ni mawazo mapya kutoka mtu/taasisi yo yote ambayo muombaji wa huduma hiyo anaamini kwamba itampatia mawazo mazuri ya kumfanya asonge mbele dhidi ya changamoto zinayokukabili. Na lengo la ushauri ni kupata mawazo mbadala au njia ya kuepukana/kukabiliana na changamoto au mzigo wa muathirika. Mara nyingi ushauri umfanya mshauriwa kupata faraja na imani na kujisika katika hali ya kawaida kimawazo na kupata nguvu mpya.
Changamoto ni jambo lo lote lililo mbele yako ambalo linakusumbua na unaliona ni kikwazo katika mustakadhali wa maisha yako, hivyo kuhitaji msaada dhidi jambo husika kutoka kwa mtu/ taasisi unayemwamini/unayoiamini. Changamoto mara nyingi uletwa na mabadiliko ya kimazingira au watu wanakuzunguka hii ni tafsiri fupi, kwa hapo mbele tutapata tafsiri nyingi na rasmi. Kihistoria changamoto katika ndoa zilianzia katika Bustani ya Eden baada ya Hawa kukaidi maagizo ya Mungu aliyoambiwa na mmewe Adam ya kutokula tunda la mti wa katikati ya Bustani ya Eden.
Ndoa ni muunganiko wa hiari baina ya mwanaume/mvulana na mwanamke/msichana kuwa mme na mke kwa lengo la kuunda familia. Muunganiko huu ni kawaida urasmishwa ki-dini, kiserikali na ki-mila. Kihistoria ndoa ya kwanza katika dunia hii, ilikuwa baina ya binadamu wa kwanza katika sayari yaani; Adam na Hawa katika Bustani ya Eden. Lengo kuu ikiwa ni kumuondolea upweke Adam katika Bustani ya Eden kwa Mungu kuamua kumpatia anayefananaye.
Uchumba ni mahusiano ya karibu sana baina ya mwanaume/msichana na mwanamke/msichana ambao unafahamika na wazazi wa pande zote kwa lengo la kufunga ndoa kwa maridhiano ya wawili hao.
MADHUMUNI YA KUUNDWA KWA BLOGU HII
Madhumuni ya blogu hii ni kutoa ushauri wa kitaalamu wa namna sahihi ya kukabiliana na changamoto zinazojitoka kila kukicha katika tasnia hizi za ndoa na uchumba katika sayari yetu hii dunia. Ushauri wa namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ndoa na uchumba kwa njia ya barua pepe kupitia anuani pepe ya mshauriwa.
Hapa mbele, nategemea kuwa nitakuwa natoa makala ya masuala ya afya na usimamizi wa biashara. Lakini hii itategemea zaidi na ushauri, maoni na mahitaji ya wasomaji wa Blogu hii.
Pia kwa kupitia blogu hii, tutatoa vitabu na majarida mbalimbali kwa njia mtandao na chapisho na Ili kupata makala husika utalazimika kuchangia kidogo.

CHANGAMOTO ZILIZO KATIKA NDOA NA UCHUMBA
Changamoto katika ndoa na uchumba zinaweza kugawanywa katika Makundi makuu mawili kwa mtazamo wa visababishi/vyanzo vya changamoto-
Ø  Zinazoletwa na watu wanaowazunguka.

Ø  Zinazoletwa na wao wenye.

Ø  Zinazoletwa na watu wanaowazunguka na pamoja na wao wenyewe
Changamoto zote hizo zote kila moja utatuzi wake umekuwa mgumu sana kwa sababu taasisi za kidini ambazo ndio mtatuzi mkuu wa changamoto hizi zinahitaji kusaidiwa na Blogu hii itafanya kazi hii ya usaidizi. Na pia baadhi ya masheikh na wachungaji wamekosa maadili yaani; usiri wa matatizo wanayoletewa na waumini wao. Pia marafiki na ndugu wengi wamekuwa hawana msaada, badala yake wamekuwa watoaji wakubwa wa changamoto za wanadoa na wachumba na inakuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa na uchumba mwingi.
 Kwa kupitia blogu hii utapata ushauri wo wote utakaohitaji katika masuala ya ndoa na uchumba na daima itabaki siri baina yako na mshauri wa Blogu hii.
MADHARA YANAYOLETWA NA CHANGAMOTO KATIKA NDOA NA UCHUMBA
Ø  Taraka/Kuacha.

Ø  Watoto wa mitaani.

Ø  Kukata tamaa ya maisha.

Ø  Kujinyoka na kujiua kwa sumu/risasi.

Ø  Kuua watoto.

Ø  Utoaji Mimba.

Ø  Uasi wa kupitiliza .n.k.
USHAURI
Napenda kukushauri kwamba kwa kusoma makala za Blogu hii, ambazo nategemea kuwa nitakuwa nazitoa kwa juma mara moja utapata mbinu muafaka za kukabiliana na changamoto zinazoletwa na matatizo ya kimahusiano katika ndoa na uchumba.
Mnakaribishwa kuomba ushauri wa changamoto zinazowakabili katika masuala ya ndoa na uchumba kwa kupitia e_mail yangu ya fkmwamoto@gmail.com

No comments:

Post a Comment