Wednesday 28 May 2014

MAMBO 4 YANAYOATHIRI MAKUZI YA WATOTO

Katika hali inayokubali katika jamii zetu, mtoto ni matokeo ya wawili waliyokubaliana kuishi kama mke na mme baada ya kufunga ndoa. Japo mara nyingine watoto wanapatikana nje ya ndoa. Leo niongee mambo manne (4) yanayoathiri makuzi ya mtoto kwa ujumla.
Makuzi ya mtoto/watoto ni jukumu la muhimu sana kwa mzazi yo yote katika jamii.

Katika tafiti mbalimbali za kisayansi makuzi anayopata mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 12 yanaakisi tabia atakayokuwa nayo katika utu uzima wake. Mambo 4 yafuatayo yanaathiri makuzi ya mtoto ni kama yafuatavyo: -
1. Kuadibisha: Hatua za kinidhamu unazochukua kwa mtoto wako huathiri malezi yake. Wataalam wa malezi ya watoto wanashauri malezi yetu yawe shirikishi kwa maana ya kwamba kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutukana watu, utoro shuleni, ugomvi n.k ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwa nini haifai kufanya jambo fulani, ili kumpatie nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo.  Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali. Pia hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kusababisha hofu kwa watoto wako, ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu hata wenzao pia.  Hata hivyo, pia kuwa mpole mno wanaweza kuendeleza ukosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wa mtoto katika jamii na shule.
2. Mazingira: Neno mazingira kwa tafsiri fupi ni vitu vyote vinavyotuzunguka hewa, miti, majengo, watu, wanyama, shule, nyumba za ibada .n.k. Mazingira ya mtoto yanaathiri ya moja kwa moja kwa mtoto hasa ya nyumbani na shuleni. Muda mwingi wa makuzi ya watoto hutumika nyumbani na shuleni. Mtoto anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. mambo hayo uathiri moja kwa moja utazamo wa mtoto wa kimaisha. Pia mtoto ambaye anasoma shule ambayo kila saa anakosa amani kutokana na kutishiwa kupigwa na walimu au wanafunzi wenzie hujengewa hali ya kuwa na wasiwasi na kutopenda kwenda shuleni na shule.
3. Mawasiliano: Mtoto ashirikishwe katika baadhi ya maamuzi ya ki-familia kama vile masuala ya chakula, vinywaji, maongezi n.k. Ninaposema kushirikishwa katika suala ya chakula ni katika hali ya kujenga tabia ya ushirikishwaji na kumpa uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake. Pia katika maongezi nina maana mtoto sema jambo lo lote ni muhimu kumsikiliza na siyo vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele. Tabia hiyo, itamsaidia kwa kumpatie uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.
4. Malezi:  Mfumo wako wa malezi unaweza kumjenga mtoto wako au kuharibu. Kuweka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo huwajengea hali ya kujisikia kuathaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo  kuwaongezea furaha na amani. Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya Imani ya kupendwa imejengwe kwenye akili zao.
Kwa hiyo, wazazi tuna jukumu kubwa sana katika kujenga watoto wetu kisaikologia katika umri wa miaka 0 hadi miaka 12. Kumjenga mtoto baada ya miaka 12 na kuendelea inakuwa vigumu sana, japo inaweza kumbadilisha.
Jiunge na blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ili UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO YA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA. Maoni na ushauri mbalimbali yanakaribishwa. Karibu PAMOJA TUSONGE MBELE.


No comments:

Post a Comment