Monday 19 May 2014

CHANGAMOTO ZINAZOSABABISHWA NA WANANDOA WENYEWE SEHEMU YA 2

Katika makala ya kwanza tulijadili jinsi kutoelewana/mawasiliano kwa wanandoa wenyewe kunavyosababisha changamoto/migogoro katika ndoa. Leo tutajadili jinsi Usaliti, Udanganyifu, Uchoyo, Kukosa maadili, Uchafu na kufichana taarifa za muhimu (Kabla na ndani ya ndoa), nakadhalika.
Usaliti: Katika mtazamo wa kindoa ni kitendo cha mwanandoa kutoka nje ya ndoa yaani; kufanya uasherati. Sababu kubwa za usaliti ni tamaa ya kimwili na ngono, kutoelewana katika ndoa, ulevi, ugonjwa wa muda mrefu wa mmoja wa wanandoa, marafiki n.k.
Katika sababu zote tajwa hapo juu inayotawala sana katika kusababisha usaliti ni tamaa ya kimwili na ngono. Yaani; kutokana na tamaa ya vitu ambayo mara nyingi wanandoa hawana uwezo wa kuvilimiki vitu fulani kwa mfano; nguo za thamani, vito vya thamani, kujipendezesha, chakula n.k mara nyingi hujikuta wakiingia katika usaliti kwa lengo la kujipatia kipato, ili kukidhi tamaa za kimwili. Usaliti wa kingono unatokana ya tabia au mapungufu kimahusiano ya kindoa ambayo sababu zake kutoelewana kimwili. Kubaliana na mgogoro huu ufafanuzi wake upo kwemye makala ya blogu nitakayoitaja hapa chini.
Ulevi ni moja ya sababu ya wanandoa wengi kutoka nje ya ndoa kwa sababu ulevi hupunguza utashi wa maamuzi kwa baadhi ya watu.
Marafiki mara nyingine hushawishi baadhi ya wanandoa wasiyokuwa na misimamo kutoka nje ya ndoa kwa tamaa ya mahitaji ya kimwili.
Udanganyifu: Ni tabia ya kutokuwa mkweli katika kauli na vitendo. Tabia hii, si tabia ya asili ni tabia inayotokana na malezi. Tabia hii, katika ndoa si nzuri kwa sababu udanganyifu husababisha wanandoa kutoamini.
Uchoyo: Ni tabia ya kutopenda kutoa. Tabia hii, inatokana na malezi. Tabia hii, husababisha wanandoa mara nyingi kutengwa na wanandugu na marafiki na jamii inayowazunguku.
Kukosa maadili: Maadili ni tabia zinazokubalika katika jamii. Yaani; mambo yanayokubalika katika jamii kama vile kuheshimiana kwa rika, lugha isiyo ya matusi. Kwa kifupi ni utii wa mila na desturi. Tabia hii ya kukosa maadili ni zao la malezi. Kwa hiyo, kukosa maadili ni kwennda kinyume na mila na desturi za jamii kama vile kutokuheshimu wakwe, mme, tabia za matusi, dharau za wazi n.k.
Uchafu: Ni tabia ya kutopenda usafi. Tabia hii, inaweza kuwa ya asili au ikitokana na malezi. Tabia hii, inaleta sana migogoro katika ndoa nyingi bila kujali tabia hii, iko kwa mwanaume au mwanamke. Tabia ni mbaya sana kwa sababu ni rahisi kupata magonjwa kwa wanandoa na watoto.
Kufichana taarifa muhimu ( kabla na ndani ya ndoa): Taarifa muhimu ambazo wanandoa wanapaswa kujulishana kabla ya ndoa ni kama vile; magonjwa ya kiukoo miongoni mwa wanandoa, uzazi wa kabla ya ndoa, n.k. Taarifa muhimu kupeana ndani ya ndoa ni kipato, majukumu yo yote nje ya yale ya wanandoa, mipango ya kimaendeleo kama vile ujenzi wa nyumba n.k. Kipengere hiki, kina changamoto nyingi ambazo mbinu za kuzikabili zimefafanuliwa zaidi kwenye makala inayopatikana kwenye Blogu yangu nyingine inayoitwa http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ambayo wenye uwezo wa kuingia ni wale tu ambayo wametimiza masharti ya Blogu husika. Masharti yako ni kutuma TZS. 10,000.00 kwenye 0784190882 airtel money na baada yapo nitumie anuani pepe yako ya google, kama una ni vizuri ukafungua.
Visababishi vyote hivyo hapo juu, vinaweza kuepukika iwepo wanandoa wenyewe wataamua/ watadhamiria kufanya hivyo. Madhara yatokanayo na changamoto katika ndoa yametajwa kwa makala yangu ya utambulisho wa blogu, ili kuiona makala hiyo bofya kwenye maandishi ya bluu.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.

No comments:

Post a Comment