Saturday, 24 May 2014

CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO ZINAZOLETWA NA WATU WENGINE WASIYOWANANDOA

Napenda kuwashukuru wale wote walionitumia ujumbe kwa ushauri na maoni. Leo nitazungumzia changamoto zinazosababishwa na watu wengine wasio wanandoa kama nilivyosema kwenye makala ya utambulisho wa blogu hii. Kwa sababu wanandoa wanaishi katika jamii, ndugu wa karibu na marafiki. Hawa wanajamii, ndugu wa karibu na marafiki wanakuwa ni chanzo cha changamoto nyingi katika ndoa kutokana na wanandoa kutokuwa na msingi imara wa ndoa yao.
Baadhi ya sababu zinazosababisha changamoto katika ndoa na watu wengine wasiyo wanandoa ni kama zifuatazo: -
Watoto: Watoto ni mibaraka katika ndoa, lakini mara nyingine huleta migogoro katika ndoa kutokana na kutoelewana wanadoa kuhusu  kuwaadabisha watoto wao na mambo mengine ya msingi kwa ajili ya watoto. Katika suala la kuwaadabisha watoto mara nyingi hutokea mmoja ya mzazi kumgombeza mwenza inapotokea mtoto anaadhibiwa na mmoja wa wazazi kwa sababu ya wawili hao kutokuwa na msimamo mmoja kuhusiana na malezi ya watoto wao. Na suala hili husababisha watoto kujenga chuki kwa mzazi anayewaadisha na upendo kwa yule anayewatetea.
Ndugu wa wanandoa: Mara nyingi hutokea wanandugu kama vile mawifi, mashemeji, wakwe nakadhalika kuwa na sauti sana kwenye masuala ya ndoa ya ndugu yao. Mambo yanayosababisha migogoro kutoka kwa wanandugu ni hutegemezi  kwa mmoja wa wanadoa. Mara nyingi ndugu hutaka kuendelea kuwaongoza wanandoa kuhusu suala la matumizi ya pesa na kusahau kwamba masuala hayo inatakiwa yaongozwe na wanandoa wenyewe kwa kuzingatia vipaumbele vyao. Hii huleta migogoro sana kwa sababu wanandugu kutotaka kutambua ushrikikishwaji wa mkewe/mmewe katika suala la misaada pande zote mbili za kwa mkewe/mmewe na kwao pia.
Kazi: Kutokana na kutumia muda mwingi sana kazini mara nyingi wanandoa wengi hujikuta wakiwa hawana muda wa kuongea na kupanga mipango muhimu ya kimaendeleo,  malezi ya watoto wao na mambo ya unyumba pia. Kutokana kutingwa na kazi nyingi wanandoa wengi hujikuta wakimaliza shida zao nje ya ndoa na kushindwa kutimiza majukumu yao ya msingi kiunyumba nyumbani kwa visingizio mbalimbali.
Marafiki: Kutokana na kukosa misingi imara, ndoa nyingi zinaangukia mikono mwa marafiki kutokana na wanandoa wenyewe kukosa maadili na kutoa siri za ndoa kwa marafiki. Hii, hutokea kwa lengo la kuomba ushauri kwa marafiki zao ambao mara nyingi huwa si marafiki wema, uwazunguka na kuwasaliti na hata kupinduka ndoa za marafiki wao.
Watumishi wa nyumbani: Mara nyingi kutokana na kukosa umakini katika masuala muhimu ya kinyumba ndoa nyingi hujikuta zikiyumbishwa na watumishi wa nyumbani wa kiume na wakike kutokana na wanandoa wengi kukosa umakini, uaminifu na tamaa za ngono. Umakini hukosekana kwa kumpa mtumishi majukumu wengi yasiyostahili kupewa mtumishi kama vile usafi wa chumbani, kutandika kitanda  nakadhalika.
Mali: Mara nyingi mali husababisha ndoa nyingi  kudumu pasipo uimara wo wote  kwa mmoja wa wanandoa kuwa mtumwa wa mali za mmoja wa wanandoa. Mara nyingi mali husababisha wanandoa wengi kuwa na tamaa ya kutoka sana nje ya ndoa kwa sababu kwa kutumia mali hiyo wanakuwa na uwezo wa kumnunua mwanamke/mwanaume yo yote na kufanya nae ngono  na hivyo kusababisha ndoa kukosa heshima. Mara nyingine kuna wanandoa wanaingia kwenye ndoa na watu wenye mali kwa lengo la kuchota mali kwa njia ya kudai taraka muda mfupi baada ya ndoa kwa visingizio mbalimbali kwa kwenda mahakamani kudai taraka ambao kisheria mali iliyochumwa kipindi cha ndoa hugawanywa kati yao.
Ili kupata maarifa ya kukabiliana na migogoro mbalimbali inayojitokeza katika taassis hii, kuwa mwanachana wa blogu ya http://mkombozi-mahusiano.blogspot.com ambayo huingiaji wake ni kwa kuzingatia taratibu zilizoelezwa kwa kwenye makala zangu zilizotangulia.
Jiunge na blogu tajwa hapo UPATE MAARIFA YA KUPUNGUZA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO, TUJENGE TAIFA.IMARA.


No comments:

Post a Comment